Wakenya waandamana kuwakumbuka Gen Z waliouwawa
25 Juni 2025Waandamanaji hao waliojitokeza kwa wingi, walipeperusha bendera za kenya na picha za waliouwawa katika maandamano ya mwaka uliopita, licha ya hofu kwamba huenda wakakabiliwa na nguvu kubwa ya polisi na wahalifu wanaodaiwa kufadhiliwa na serikali.
Takriban watu 60 waliuwawa mwaka jana na maafisa wa polisi ndani ya wiki kadhaa za maandamano ya kupinga rushwa, ongezeko la kodi na hali mbaya ya kiuchumi kwa vijana wa Kenya.
Gen-Z Kenya waandamana kuwakumbuka wenzao 60 waliouawa 2024
Wanaharakati na familia za waathiriwa hao wameitisha maandamano ya amani kuwakumbuka waliouawa. Hata hivyo baadhi ya wanaharakati walitoa wito kwa waandamanaji kufika hadi katika ikulu ya rais William Ruto.
Shule na biashara mijini zilifungwa kufuatia wasiwasi wa kutokea machafuko makubwa.