Maelfu ya Wairan waandamana kuipinga Israel
20 Juni 2025Maelfu ya watu katika mji mkuu wa Iran, Tehran,wameandamana kuipinga Israel baada ya sala ya Ijumaa. Waandamanaji hao wametoa kauli za kuwaunga mkono viongozi wao. Kwa mujibu wa waandaaji, Ijumaa ya leo ilikuwa siku ya mshikamano kwa Wairani, ambapo maandamano yalifanyika pia kwenye miji mingine kote nchini humo.
Wakati huo huo, nchi za Ulaya zinafanya juhudi ili kuleta suluhisho la kidiplomasia katika vita vya Iran na Israel. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema wawakilishi wa Ulaya wanakutana mjini Geneva na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran. Israel imesema inatazamia mawaziri hao wa mambo ya nje wa Ulaya watakuwa na msimamo thabiti dhidi ya Iran na kuitaka kuachana kabisa mpango wake wa nyuklia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema mashambulizi ya Israel yalikusudia kuziuwa juhudi za kidiplomasia kati ya nchi yake na Marekani.