Maelfu waandamana Marekani kupinga sera Trump
6 Aprili 2025Miongoni mwa sera zake zinazopingwa na waandamanaji hao ni pamoja na za uchumi, kupunguzwa kwa wafanyakazi wa serikali, ushuru, uhamiaji na haki za binadamu.
Maandamano hayo ya Jumamosi yamefanyika katika maeneo 1,200 ya majimbo yote ya Marekani. Waratibu wake ni pamoja na mashirika ya kiraia, vyama vya wafanyakazi, watetezi wa mapenzi ya jinsia moja na wanaharakati wa uchaguzi.
Donald Trump amewakasirisha Wamarekani walio wengi kwa hatua yake zake kali za kupunguza serikali na kwa kuwalazimisha raia kufuata maadili ya kihafidhina, pamoja na kuzishinikiza vikali hata nchi rafiki kwa Marekani katika masuala ya mipaka na biashara. Waratibu wa maandamano hayo ya amani wamesema walitarajia kuwa yangehudhuriwa na watu 20,000 lakini waliojitokeza ni zaidi ya idadi hiyo.