SiasaBangladesh
Maelfu ya waandamanaji Bangladesh wadai uchaguzi mkuu
28 Mei 2025Matangazo
Hayo ni wakati hali ya kutoridhika ikiongezeka dhidi ya serikali ya mpito iliyoteuliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina mwezi Agosti.
Wanaharakati kutoka makundi matatu yenye uhusiano na Chama cha Bangladesh Nationalist, au BNP, kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Khaleda Zia walikusanyika mitaani nje ya makao makuu ya chama chake, chini ya ulinzi mkali.
Soma pia: Bangladesh yasitisha usajili wa chama cha Hasina
Maandamano ya Jumatano yamefanyika baada ya wiki kadhaa za mvutano wa kisiasa baada ya kiongozi wa mpito na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Muhammad Yunus kutishia kujiuzulu na mkuu wa majeshi mwenye ushawishi mkubwa akatangaza hadharani kuunga mkono uchaguzi kufanyika mwezi Desemba.