Maelfu wafurika kutoa heshima ya mwisho kwa Papa
23 Aprili 2025Matangazo
Vatican imefungua rasmi shughuli ya kuuaga mwili wa Papa kwa siku tatu kuanzia leo Jumatano, kabla ya mazishi yaliyopangwa kufanyika Jumamosi.Soma pia:Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili Indonesia
Jeneza la mbao alilolazwa kiongozi huyo limewekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro likiwa limewekewa ulinzi maalum. Usalama umeimarishwa huku shughuli zikisimama katika mji wa Rome.
Maelfu ya watu wanatarajiwa kuendelea kumiminika kwa siku kadhaa zijazo kwa ajili ya kumuona kwa mara ya mwisho kiongozi huyo wa kiroho. Wakati huo huo, makadinali wamekutana kukamilisha maandalizi ya mazishi na kupanga baraza la kumchagua Papa mpya.