Maelfu waandamana Iran kuwaunga mkono Wapalestina
28 Machi 2025Matangazo
Yamefanyika huku Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei akiwataka watu wa Iran kuandamana dhidi ya kile alichokiita hila za maadui.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP ni kwamba umati wa watu walipeperusha bendera za Iran na Palestina pamoja na zile za kundi la wanamgambo wa Lebanon wa Hezbollah wakiwa na mabango ya kuikejeli Marekani na Israel.
Mamlaka ilitoa wito kwa Wairani kujitokeza kwa nguvu kwa ajili ya maandamano dhidi ya Israel, ambayo inamtaja kama adui mkubwa wa Iran ambayo haimtambui na ambayo inaitaja kuwa ni yenye "utawala wa Kizayuni".
Hata hivyo, Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani na Israel kwamba inaliunga mkono kundi la wanamgambo wa Hezbollah la nchini Lebanon.