SiasaVenezuela
Maduro asema yuko tayari kwa mapambano na Marekani
6 Septemba 2025Matangazo
Maduro amesema hayo katika muktadha wa mvutano unaoongezeka kati ya Marekani na Venezuela. Rais wa Venezuela amesema kwa sasa nchi yake imo katika hatua ya kisiasa.
Hata hivyo ameeleza kuwa ikiwa Venezuela itashambuliwa kwa njia yoyote basi chi hiyo itaingia katika hatua ya mapambano ya silaha. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, ndege mbili za kijeshi za Venezuela ziliruka karibu na manowari ya Marekani, kitendo ambacho Marekani imekiita kuwa ni uchokozi mkubwa.
Marekani imeeleza manowari hiyo ipo kwenye sehemu ya kimataifa na imeitaka Venezuela iache kuzuia juhudi za Marekani za kupambana na walanguzi wa mihadarati.