MuzikiUlaya
Madonna aadhimisha miaka 67 kwa mbio za farasi za Italia
17 Agosti 2025Matangazo
Madonna alitazama mbio hizo kutoka kwenye jumba la kifahari la Palazzo Pannocchieschi d'Elci, linaloangalia uwanja wa Piazza del Campo. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, aliendelea na sherehe hizo baadaye katika hoteli ya nyota tano iliyoko katikati ya mji wa kihistoria wa Siena. Hii si mara ya kwanza kwa Madonna kusherehekea siku yake ya kuzaliwa nchini Italia. Mwaka jana, alisherehekea huko Pompeii, mji wa kale karibu na Naples, maarufu ambao ulifukiwa wakati wa mlipuko wa Mlima Vesuvius ikikadiriwa takribani miaka 1946 iliyopita.