Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti ya Ujerumani hii leo:
26 Januari 2004Matangazo
Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG, kuhusu jitihada ya Ujerumani ya kuzipatanisha pande za Israel na kundi la upinzani la kipalestina katika swala la kubadilishana wafungwa, linaandika: Jukumu linaloshikiliwa na serikali ya Berlin kuhusiana na hali katika mashariki ya kati, mara nyingi hukadiriwa juu sana, lakini kile ambacho kimepatikana sasa, kinasisitiza ukweli wa mambo ulivyo, yaani utayarifu wa Ujerumani wa kutoa mchango wa kisiasa na wa kiutu, ambao unafahamiwa na kuaminiwa na pande zote mbili. Naam, hii ni hatua mpya ya mafanikio ya siasa za Ujerumani kuelekea mashariki ya kati.
Gazeti mashuhuri la hapa jijini Bonn, GENERAL-ANZEIGER, linatoa maoni kama hayo kuhusu mada hii, linapoandika: Serikali ya Ujerumani inaweza kujivunia hali kwamba, inachangia kwa njia ya diplomasia ya idara ya ujasusi kuwapunguzia machungu nyoyoni jamaa wa familia za Israel na Lebanon. Funzo linalopatikana kutokana na utayarifu huu uliotangazwa mwishoni mwa wiki, pia unashuhudia wajibu muhimu unaoshikiliwa nyuma ya pazia na Iran.
Endapo Iran pamoja na Syria, zingeacha kulihami kundi hili la Hisbollah, basi pangepatikana matumaini kwa kiasi fulani cha kuwa na mafanikio. Lakini inaelekea hali inaonekana vingine.
Wasiwasi kuhusu swala hili, unahaririwa na gazeti la mji wa Dortmund, RUHR-NACHRICHTEN, linapoandika: Inabidi kusubiriwa kuona kama ubadilishanaji huu wa wafungwa, utakuwa wa faida kwa muda mrefu. Kundi hili la kigaidi la Hisbollah, linasherehea tangu muda mrefu kuwekwa katika hadhi nyingine kama ni ushindi wa propaganda. Lakini huenda hisia hizi zikawa za hatari kwake, wakati Israel inapokadiria hali hiyo kama ni ishara ya udhaifu, ambayo ingelirejesha kundi hili tena katika makabiliano ya kisiasa.
Gazeti lingine la kusini mwa Ujerumani, STUTTGARTER NACHRICHTEN, kuhusu kutakiwa ajiuzulu Mkrugenzi-mkuu wa shirika la ajila la Ujerumani, Florian Gerster, linakadiria hatima yake kwa kusema: Mtu ambaye hutazamwa na wengi ni mwenye kujigamba, amechelewa kupata mshirika wa kumuunga mkono. Badala yake kiongozi huyu wa zamani wa shirika la ajira, aliendelea kushikilia kwamba, hakuwahi kufanya kosa katika kushikilia hatamu zake.
Gazeti mashuhuri kibiashara la mji wa magharibi wa Düsseldorf, HANDELSBLATT, linatoa maoni mengine juu yake kwa kuandika: Kikwazo kikuu kwenye njia kuelekea kuufanyia mageuzi uongozi wa shirika la ajira, sio ni kwa kuwa mkurugenzi-mkuu huyu alikuwa ni mtu wa kujigamba. Bali ni hatari kwamba, mageuzi ya kisiasa yangemfanya kuwa ni mhanga, kulingana na masilahi ya vyama vya upinzani. Kuachishwa kazi Gerster huenda kukazusha hali ya waziri wa uchumi Clement kukabiliwa na kashfa mnamo mwaka huu wa 2004. Mada hii pia inazingatiwa na gazeti mashuhuri kimataifa, DIE WELT, linapoandika: Kwanza yatabidi kufanywa mageuzi ya kukarabati uongozi wa shirika hili, kwa nia ya kusimamiwa bora kazi za maofiwa wahusika.
Na pili atabidi sasa kuchaguliwa mkrugenzi-mkuu mpya, ambaye atakuwa na kipaji cha kushikia usukani mfumo wa mageuzi.
Tunafikia wisho wa uhariri wa leo katika magazeti ya Ujerumani, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la kusini mwa Ujerumani, SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, kuhusu mada hii, linaloposema: Ni wakati Kansela Schröder pamoja na waziri wake wa uchumi Clement, watakapofanikiwa kupata mkurugtenzi-mkuu mpya, ambapo itazuiliwa hali ya Folria Gertser kuhisi kwamba, hakuachishwa kazi kwa hiari yake. Kitisho cha upande wa upinzani cha kuchukua hatua katika tume ya upatanishi, kinaelekea hakitafanikiwa. Kwani sababu zilizolepekea kufutwa kazi kwake, zimeshatangaza rasmi hadharani. Hata hivyo tatizo kuu linabakia sasa katika upande wa serikali, kwa sababu uchaguzi wa mkurugenzi-mkuu mpya wa shirika hili kuu la ajira la Ujerumani, sasa utadumu muda mrefu zaidi.

Matangazo