Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti ya Ujerumani hii leo
4 Machi 2004Matangazo
Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER RUNDSCHAU, kuhusu uamuzi uliopitishwa na mahakama ya katiba ya Ujerumani katika mji wa Karlsruhe, linaandika: Kifungu cha 13 cha sheria inayohusika kinachodfai kuchukuliwa hatua watu wanaoshukiwa ni wahalifu katika makazi yao, kinawanyima watu hao haki ya kuishi huru. Mahakama hiyo inasema usikilizaji huo wa chini kwa chini wa simu, hautachangia chochote katika kupambana na vitendo vya kihalifu. Wengi miongoni mwa wajumbe wa senet ya mahakama hiyo, wameshindwa katika dai lao la kushikiliwa sheria hiyo, iliyopitishwa miaka sita iliyopita, pia kwa kukubaliwa na vyama-ndugu vya upinzani vya CDU na CSU pamoja na FDP. Lakini isisahauliwe kwamba, si kifungu hicho cha sheria cha 13 pekee kinachohusika, bali hasa ni nia ya kufanya mageuzi ya kuwachukulia hatua wahalifu.
Mada hii inachambuliwa pia na gazeti la Kolon, KÖLNER ANZEIGER, linapoandika: Anayeridhika hasa na uamuzi huu wa mahakama ya katiba mjini Karlsruhe, ni waziri wa zamani wa sheria wa Ujerumani Bi.Sabine Luetheuser Schnarrenberg, ambaye pamoja na wenzi wake wawili katika chama cha FDP, alijiuzulu wadhifa wake, baada ya kushindwa kwenyse uamuzi uliopitishwa na mahakama hiyo mwaka 1995. Wakati huo waziri huyo wa zamanji alihurumiwa na wengi katika chama chake. Lakini leo inadhihiri kwamba, wanasiasa hao watatu walishikilia msimamo wa haki kuhusu uamuzi huo wa kusikilizwa simu za watu katika fleti zao.
Gazeti lingine la kusini mwa Ujerumani, SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, kuhusu mada hii linasema: Hatimaye mahakama ya katiba imechukua hatua ya kutoa mafunzo ya namna ya kuoanishwa shughuli za kisiasaa na za upitishaji sheria. Mahakama hii imechukua hatua hii kupinga kukiukwa kwa uhuru wa maisha ya faragani, ambao unabidi kuhakikishwa na dola. Uamuzi huo unapinga nia hiyo ya kusikilizwa chini kwa chini simu za washukiwa wa kihalifu kama mkakati wa kupambana na uhalifu. Isitoshe, uamuzi huo wa zamani unakwenda kinyume cha hisia za kisiasa na dhidi ya sheria za usalama.
Gazeti mashuhuri la hapa jijini Bonn, GENERAL ANZEIGER, linakamilisha mada hii kwa kuandika: Mshindi mwingine katika uamuzi huu wa mahakama ya katiba ni dola lenyewe. Senet ya mahaka hii imepitilia uzito hatua mbili muhimu, hatua ya kwanza ikiwa ni kulindwa uhuru wa kibinafsi katika makazi ya washukiwa. Hakuna mtu aliye na haki ya kusikiliza kwa siri simu za watu katika makazi yao. Na pili senet hii inashikilia wahalifu kuchukuliwa hatua za adhabu za hadi miaka mitano.
Kuhusu mashindano ya kuwania wadhifa wa rais mpya wa marekani kwenye uchaguzi mkuu mwezi Novemba nchini Marekani, gazeti la mji wa Würtzburg MAIN-POST, linaandika: John Kerry hawezi kutazamwa ni mgombea bora kabisa na mwenye kipaji cha kutawala, hata hivyo, anaaminiwa ana uwezo wa kuunganisha wapinzani katika siasa za ndani: Alikuwa zamani ni mwanajeshi kama mshindani wake Wesley Clark, ni mwenye kufuata mkondo wa kiliberali na mwenye kutilia uzito thamani ya huduma za kijamii na mtaalamu wa maswala ya nje. Sifa hizi zinamfanyaa kuwa mgombea wa wadhifa wa rais anayefaa dhidi ya mshindani wake rais Bush. John Kerry pia anasfika kwa sababu anatetea harakati za kuzuwia hujuma za kigaidi dhidi ya marekani na kufanyiwa mageuzi mfumo wa huduma za kijamii nchini humo.
Gazeti la MITTEL-BAYERISCHE ZEITUNG, linatukamilishia uchambuzi wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani, linapobiri kuhusu mada hii: kile kinachosuburiwa sasa kwa hamu na wengi, ni kuona jinsi matokeo ya uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani yatakavyokuwa ya kama John Kerry atakuwa ndiye mshindi na kuwa rais mpya, au labda George W.Bush atashinda na kusalia madarakani.

Matangazo