Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti ya Ujerumani hii leo
12 Julai 2004Kuhusu warsha wa baraza la mawaziri la chama-tawala SPD, gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, linaandika: Hisia za mafungamano za mawaziri zinanuwia kumhakikishia Kansela jinsi wanavyojitahidi kuzingatia roho ya timu moja kama hali ilivyo katika mchuano wa kadanda. Lakini swali muhimu ni kama mafungamano haya ya timu moja yataweza kudumu muda mrefu? Sababu ni kwa kuwa hali ndani ya chama-tawala SPD, si ya kutia moyo sana wakati huu, hasa ikikumbukwa kwamba, sehemu ya mageuzi ya huduma za kijamii ya serikali, itaweza kuhisiwa na raia si mapema kuliko mwaka ujao wa 2005. Wengi wanasubiri kwa hamu kuona jinsi miradi minne muhimu itakavyotekelezwa na serikali: mradi wa kwanza ni ule wa mageuzi katika masoko ya ajira, mwingine ni mageuzi katika malipo ya uzeeni, tatu mageuzi katika tiba ya meno na hatimaye mageuzi ya bima ya huduma za wastaafu.
Gazeti lingine la kusini STUTTGARTER NACHRICHTEN, kuhusu mada hii linakumbusha: Kansela ameitisha warsha huu maalum, pindi kuwaelekeza mawaziri wake malengo ya mpango wake wa mageuzi. Sababu ni kwa kuwa sasa kinaingia kipindi muhimu cha kupitisha maamuzi ya kuaminika. Hata ikiwa wakati huu serikali haina peremende za kuwatuliza walipaji kodi, wapigaji kura wasije wakafanya kosa la kumkadiria vibaya Kansela katika siasa na malengo yake. Kwani, ameshawatolea ahadi raia kutekelezewa kipindi cha kwanza cha mageuzi ya huduma za kijamii kuanzia mwaka ujao wa 2005. Lakini inaweza kusubiriwa kwa hamu tu kuona jinsi serikali ya muungano kati ya vyama vya SPD na Kijani, utakavyotekeleza kwa kweli malengo hayo.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani CDU, Angela Merkel, ametoa matamshi makali ya kukosoa jinsi chama chake pamoja na chama-ndugu cha mkoa wa bavaria cha CSU, vilivyoshindwa katika kupiga makasia ya kisiasa kwa pamoja.Kuhusu mada hii, gazetzi la MANNHEIMER MORGEN, linaandika: Mtu akisikia matamshi hayo anaingiwa na swali muhimu, kama kwa kweli vyama-ndugu hivi vya kikonsavativ vinaweza kuwa uwezekano wa busara wa kushikilia hatamu za serikali badala ya wasocial-demokratiks. Angela Merkel anakosoa kwa haki hatari ya vyama-ndugu hivi kutilia chumvi na kuhisi kama vinaaminiwa na wapigaji kura. Anaeleza hofu ya raia wengi kupoteza imani ya kutekelezewa masilahi yao ya kiuchumi na huduma za kijamii. Mwenyekiti wa CDU ametoa matamshi hayo ya kujikosoa binafsi, kwa sababu anahisi kwamba, endapo chama chake pamoja na chama-ndugu vingekanyakua ushindi na kuunda serikali mpya, vingekuwa vikifarakana kila kukicha kuwanaia madaraka.
Tunakamilisha uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la magharibi SAARBRÜCKER ZEITUNG, kuhusu mada hii: Wakati huu wakristian-demokrats, wanafurahia hali ya kuwa na wingi wa kura katika bunge la serikali za mikoa, inayowafanya kuingiwa na hisia ya kuamua mwelekeo wa siasa za Ujerumani kwa jumla. Kwa kweli nia hii isingewahangaisha sana wapigaji kura, lakini itabidi kufafanuliwa zaidi kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ujao. Inavibidi vyama-ndugu kuwaeleza kinaganaga wapigaji kura jinsi watakavyoweza kutekeleza masilahi yao ya kiuchumi na huduma za kijamii, endapo vingeia madarakani hii leo.