Mada muhimu zinazohaririwa na magazeti ya Ujerumani hii leo:
8 Januari 2004Matangazo
Magazeti mengi ya Ujerumani, yanatilia uzito hasa mapendekezo yaliyotolewa na chama kimojawapo cha upinzani cha mkoa wa Bavaria, CSU, ya kuchangia mpango wa mageuzi ya kodi wa serikali. Kuhusu mada hii, gazeti mashuhuiri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLGEMEINE, linaandika: Mapendekezo hayo ya CSU ya kuchangia muundo wa mfumo wa wakati ujao wa kodi, ni bora kuliko yale ya chama-dada cha CDU, kwa sababu yanaahidi mageuzi machache zaidi, ambayo yangekuwa rahisi kutekeleza. Lakini shida inayovikabili vyama-dada hivi ni kwamba, vimekuwa vikisubiri kwa muda mrefu kujibu mjadala wa mageuzi ya Kansela Schröder. Endapo Kansela ataamua kupitisha mapema sheria inayohusika mwaka ujao wa 2005, basi mwenyekiti wa CSU Stoiber pamoja na kiongozi wa kundi la CDU bungeni Merz, hawatasema tena hawana haja ya kuhangaika, wapigaji kura watabidi kusubiri hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2006.
Gazeti la mji wa mashariki wa Potsdam, MÄRKISCHE ALLGEMEINE, kuhusu mada hii linatoa mawazo kwa kuandika: Tofauti kubwa iliyoko katika ya vyama-dada vya CDU na CSU, hazikutikani katika swala la mageuzi ya kodi, bali zinakutikana katika misimamo inayohitilafiana sana.
Mawazo haya yanaungwa mkono na gazeti la jiji la Berlin, BERLINER ZEITUNG, linaposema: Hapana shaka Kansela Gerhard Schröder sasa anajikuta katika hali ya kuyafikiria mapendekezo hayo ya mwenyekiti wa CSU Stoiber. Lakini asisahau kwamba, mabilioni ya pesa, ambayo yangepatikana kutokana na mfumo mpya wa mageuzi haya ya kodi mnamo mwaka ujao wa 2005, yangenufaisha hasa ustawi wa kiuchumi, ambao katika upande wa pili, ungechangia jitihada ya kupunguza idadi ya ukosefu wa ajira, hadi ufikapo mwaka wa uchaguzi mkuu.
Gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Munich, SÜDDEUTESCHE ZEITUNG, linajishugulisha na mada nyingine kabisa kuhusu mjadala wa ni nani angefaa kuwa mgombea wadhifa wa rais mpya wa Ujerumani, kwa kuandika: Mwenyekiti wa chama cha upinzani CDU, Angela Merkel, anamtendea mwenzi wake Wolfgang Schäuble, jinsi Helmut Kohl, alivyokuwa akimtendea mwenzi wake rais wa zamani Richard von Weizsäcker, yaani kwa namna ya kumfanyia hila. Anasitasita kusema ukweli wa mambo kwamba, hamtaki awe ni mgombea wa wadhifa huu. Hii si kamwe ishara ya kipaji cha uongozi. Bibi Merkel atabidi kukubaliana hatimaye na pendekezo la mgombea wa pamoja kati ya chama chake CDU na chama-dada cha CSU.
Gazeti lingine la jiji la Berlin, TAGESSPIEGEL, kuhusu mada hii linakumbusha umbali wa kilometa 600, uliowatenganisha jana Wolfgang Schäuble na mwenzi wake chamani, Klaus Töpfer. Wakati Bw.Töpfer, mwenyekiti wa sasa wa shirika la ulinzi wa mazingira la umoja wa mataifa, alipokuwa mgeni wa rais Rau mjini Berlin, mwenzake Schäuble alikuwa mgeni wa mkutano wa CSU katika Kreuth mkoani Bavaria. Wote wawili wanakadiriwa sana ndio wangefaa kuwa wagombea wa wadhifa wa rais mpya wa vyama hivi dada. Lakini vyama vyao vinataka kupatana mgombea wao wa pamoja sio kabla ya mwezi machi.
Vyama-dada hivi vya CDU na CSU, vinanuwia kutumia mada ya Uturuki kupatiwa au kutopatiwa uwanachama katika umoja wa ulaya, katika kampeni zake za uchaguzi wa bunge la ulaya katika mwezi juni. Kuhusu mada hii, gazeti la biashara la mji wa magharibi wa Düsseldorf, HANDSELSBLATT, linaandika: Katumika kwa kampeni dhidi ya Uturuki kuweza kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya, kwa ajili ya uchaguzi wa bunge la ulaya, hili ni kosa kubwa, na mada isiyo halali, na ambayo ingehatarisha kuchanganyishwa waturuki katika maisha ya kijamii katika Ujerumani, na ambayo si ya busara kisiasa. Washirika wa magharibi, wanaihitaji sana Uturuki kupita wakati uliopita. Mtu hawezi kuigawa sehemu mbili Uturuki: katika upande mmoja kulindwa thamani yake ya kuwa mwanachama wa shirika la NATO, na katika upande wa pili, vyama vya CDU na CSU, kuzuwia uwanachama wa Uturuki katika umoja wa ulaya. Kimsingi umoja wa ulaya, umeshapitisha uamuzi wa Uturuki kuwa mwanachama wake mmojawapo, lakini iio kabla ya kutekeleza masharti yanayodaiwa, karata ya utatuzi, sasa iko mikononi mwa Uturuki yenyewe.

Matangazo