Mada muhimu zinazohaririwa na magazeti ya Ujerumani hii leo:
4 Februari 2004Matangazo
Gazeti mashuhuri la mji mkuu Berlin, TAGESSPIEGEL, kuhusu tangazo la shirika la usafiri wa reli la Ujerumani la kuwafidia abiria watakaokuwa wakicheleweshwa na treni, linaadika: Hatimaye shirika hili limewasili katika enzi ya baada ya vita vikuu vya pili vya dunia. Yaani, endapo treli fulani inachelewa, abiria anayeisubiri ana haki ya kufidiwa tiketi yake. Hadi sasa shirika hili lilikuwa likifuata sheria, iliyopitishwa mwaka wa 1908. Ukweli wa kwamba sasa yamepatikana mabadiliko, hii kwa kweli ni risala njema.
Nalo gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Munich, TAGES-ZEIITUNG, kuhusu mada hii linakaribisha risala hii kwa kuandika: Shirika la reli limeahidi kufidia kiasi ya asilimia 20 ya nauri iwapo abiria anacheleweshwa na treni za masafa marefu kwa muda wa zaidi ya dakika 60.
Lakini tangazo hili si la haki, kwani wale abiria watakaokuwa wakicheleweshwa na treni za kimkoa, hawatakuwa wakifidiwa.
Mada hii inazingatiwa na gazeti la mashariki mwa Ujerumani, MÄRKISCHE ODER-ZEITUNG, linapofichua: Tangazo hili linalofanana na kiapo, la kuwa tayari kuwafidia abiria watakaokuwa wakicheleweshwa, lina lengo la shirika hili la kuficha ukweli wa kwamba, treni zake zinachelewa mara nyingi, sio kwa sababu labda ya magari yanayovuka kwenye reli, hali mbaya ya hewa au labda mtu ambaye anataja kujinyonga kwa kuruka chini kutoka daraja ya reli, bali ucheleweshaji huu unatokana moja kwa moja na matatizo ya ndani ya usafiri yanayolikabili.
Gazeti lingine la kusini WIESBADENER KURIER, linazingatia pendekezo lililotolewa na makamu wa kiongozi wa kundi la vyama-ndugu katika bunge la Ujerumani, Friedrich Merz, linalodai kupandishwa kodi tadhmini ya bidhaa" Value Added Tax", kwa kuandika: Pendekezo hili la Merz linasikika kama ni kitzendawili, kwa sababu mwenyekiti wa chama chake cha CDU, Angela Merkel, ameshakubaliana naye tayari juu ya kiwango kinachomhuusu kila raia cha kugharamia huduma za afya. Ndio maana zinahitajika pesa za kuvigharamia, pesa ambazo haziwezi kupatikana kwa kufuatwa pendekezo lake, kama wengi katika chama chake wanavyokubaliana.
Kuhusu mada hii, gazeti la OFFENBACH POST, linasema: Inaelekea serikali imeshashindwa kulitatua swala hili, ndio maana inapita huku na kule kwa mpango wake wa mageuzi. Hii ndiyo sababu kwanini karata zinaendelea kuchangnywa kati ya vyama-ndugu vya CDU na CSU. Wakati Friedrich Merz pamoja na mwenzi wake waziri-mkuu wa mkoa wa Saarbrücken, Peter Müller, wanapoidhinisha kupandishwa kodi ya wateja, mwenyekiti Angela Merkel, anawapinga. Kwa sababu hii raia wengi wanajiuliza jinsi hatima yao na ya nchi yao Ujerumani, inavyotakikana ionekane?
Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG, linapozingatia yale mapendekezo yaliyotolewa karibuni na waziri-mkuu wa Israel, Ariel Sharon, la kupunguza makazi ya waloziwezi wa kiyahudi katika maeneo ya Ufukwe wa magharibi na Ukanda wa Gaza, linaandika: Inaelekea mapendekezo haya yanalenga kuihakikishia Israel ardhi katika maeneo ya Judea nab Samaria, shabaha ambayo inazingatiwa na walowezi wengi wanaoshikilia maadili ya kidini. Haya ni malengo ambayo hayatakubaliwa wala na upande wa Wapalestina wala wa wenye kufuata itikadi kali. Kwa hivyo, inatubidi kusubiri kuona jinsi Sharon atakavyotekeleza mapendekezo hayo katika vitendo.
Gazeti mashuhuri la mji mkuu Berlin, BERLINER ZEITUNG, linatukamilishia uchambuzi wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani, kwa kuchangia maoni kuhusu mapendekezo haya ya Sharon, linapoandika: Sharon hazungumzii juu ya ardhi takatifu, wala juu ya yale anayoamini kwamba, Israel ingeweza kulinda haki zake katika maeneo ya Wapalestina kwa kushikilia ujenzi wa makazi mapya ya wayahudi. Waziri-mkuu Sharon anazungumzia tu juu ya umahaji, ambao bado inambidi kutayarisha. Hayali wimbi la upinzani linalomkabili kutoka upande wa mshirika katika serikali yake.

Matangazo