Mada muhimu zinazohaririwa na magazeti mengiu ya Ujerumani hii leo:
3 Februari 2004Matangazo
Gazeti la ESSLINGER ZEITUNG, kuhusu mjadala unaoendelea wa kupata mikakati inayofaa katika kutekeleza mpango wa mageuzi ya huduma za kijamii, kati ya vyama-tawala vya SPD na Kijani, linaandika: Yule anayezingatia kwa makini mjadala unaoendelea wakati huu kati ya vyama-tawala dhidi ya vyama vya upinzani, ama anatikisa kichwa kwa sababu hauelewi, au anadai serikali ichukue hatua kali za kuharakisha kukamilishwa kwake. Kwani kwa sababu ya matatizo yanayobidi kutatuliwa haraka iwezekanavyo, serikali inabidi kuchukua hatua kabambe za kisiasa.
Nalo gazeti la MANNHEIMER MORGEN, kuhusu mada hii linatoa maoni: Hofu ya chama.-tawala cha SPD kuhusiana na mpango wa mageuzi, haiji bila ya kuwa na sababu zake. Ikumbukwe tu jinsi Kansela Schröder alivyopata bahati ya kupitisha mpango wake wa mageuzi ujulikanao kama "Agenda 2010" katika bunge kuu na bunge la serikali za mikoa mwaka uliopita. Lakini badala ya sifa kwa mafanikio hayo, raia wengi wanahisi athari za kwanza za mpango huu wa mageuzi ambao unakwenda kinyume cha masilahi yao. Wengi wanaghadhabishwa sana na maongozi ya serikali, lakini sio na yale yanayodaiwa na vyama vya upande wa upinzani. Mada hii pia inatiliwa uzito na gazeti la kibisshara la mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Düsseldorf, HANDELSBLATT, linapoandika: Kwa mpango wake wa Agenda 2010, Kansela aliweka msingi wa mageuzi haya mnamo mwaka uliopita wa 2003, mafanikio ambayo yalivifanya vyama-tawala vya SPD bna Kijani kutembea mkono kwa mkono katika wakati mgumu. Na hali hii huenda ikaendelea pia katika mwaka huu mpya wa 2004. Gazeti la kaskazini mwa Ujerumani,LÜBECKER NACHRICHTEN; linakumbusha: Chama-tawala SPD, hakipotezi sifa kwa sababu ya kudai mengi ambayo yanapita uwezo wa raia, bali wapigaji kura wake wa jadi wanahamaki hasa kwa sababu chama hiki kinashindwa kutekeleza kikamilifu na itakikanavyo madai yao ya huduma za kijamii. Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG, kuhusu matatizo ya nakisi yanaomkabili rais wa Marekani George W.Bush, linaandika: Nguvu za serikali mjini Washington zinategemea karibu kamili hali ya uchumi, iwapo inataka kupunguza nakisi kwa nusu mnamo kipindi cha miaka mitano ijayo. Katika mpango wake haitilii uzito umuhimu wa kupunguzwa matumizi ya serikali. Labda hali hii inatokana na ukweli kwamba, kila mwanzo wa mwaka, rais Bush anajaribu kujihakikishia ushindi kwenye uchaguzi wa rais baadaye mwaka huu, kwa kuwatuliza wapigaji kura wake. Ingekuwa muafaka, iwapo rais Bush angechukua hatua za kuridhisha dola pamoja na raia, ya kupunguza madeni.
Gazeti lingine mashuhuri la kusini mwa Ujerumani,STUTTAGARTER NACHRICHTEN, linaeleza hofu kuhusu yale maradhi ya homa ya kuku, iliyozuka katika baadhi ya nchi za Asia, kwa kuandika.
Hatari ya maradhi haya inatukumbusha hatari iliyowakabili binadamu mwaka mmoja uliopita, wakati ulipozuka ugonjwa wa hatari wa pafu kutoka China. Lakini yalipatikana haraka mafanikio ya kuukinga kabisa, hofu hiyo imeshatoweka karibu kamili. Je, tunajifunza kitu gani kutokana na maradhi haya ya kuambukiza? Tunajifunza kwamba, inatubidi kusambaza habari husika haraka iwezekanavyo pindi kuwapunguzia hofu wateja. Kwa ufupi inatubidi sote kushirikiana bega kwa bega katika kukinga maradhi, ambayo yanaelekea kuhatarisha na hata kuanmgamiza maisha yetu. Tunahitimisha uhariri wa leo katika magazeti ya Ujerumani, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la HESSISCHE/ NIEDERSÄCHSICHER ALLGEMEINE, linaposema kuhusu mada hii: Kuna fununu nyingi zinazoendelea wakati huu kuhusu maradhi haya ya homa ya kuku, lakini kile ambacho tunahitaji, ni utulivu wa kusubiri kutambua kama kwa kweli haya ni maradhi ya hatari ua la. Inavutia masilahi ya mtu kuona jinsi maofisa wahusika katika nchi za Asia, wanavyocheza karata kwa uwazi zaidi kuhusu homa hii ya kuku, kuliko wakati wa ugonjwa uliotangulia wa pafu. Ukweli huu umezusha hali ya kupigwa marufuku biashara ya nyama ya kuku barani ulaya kutoka nchi zinazohatarishwa na ugonjwa huo.

Matangazo