Mada muhimu zinazohaririwa na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo
19 Novemba 2003Linapozingatia msimamo wa kamishina wa umoja wa ulaya, Pedro Solbes, gazeti mashuhuri kimataifa, DIE WELT, linaandika: Mkataba wa kuimarisha thamani ya sarafu ya Euro umeshafariki, hata ikiwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaoshikilia kwamba, mkataba huu bado u hai. Mvutano kati ya kamishina Solbes na waziri wa fedha wa Ujerumani Eichel, katika swala la kama Ujerumani inajitahidi kuchangia ubanaji matumizi, hauruhusu uamuzi mwingine. Kwani Bw.Solbes anataka kumruhusu mwenzi wake Eichel, kubana nakisi kutovuka kiunzi cha asilimia tatu, hadi ifikapo mwaka wa 2005, lakini iwapo tu atafanikiwa kubana matumizi, kwa kiwango cha Euro Bilioni nne mwakani. Hata hivyo, waziri wa fedha Eichel, anakitazama kipimo hiki kwenda kinyume cha mkataba wa kuimarisha thamani ya sarafu ya Euro, kwani hali hii inamaanisha Ujerumani itaibidi kutafuta mikopo mipya, ili iweze kukwamua hali yake ya maendeleo ya kiuchumi.
Kuhusu mada hii, gazeti la shuguli za biashara HANDELSBLATT la mji wa magharibi wa Düsseldorf, linasema: Badala ya kuruhuru kuhangaishwa, Bw.Solbes ameamua kuichukulia hatua kali Ujerumani bila kuchelewa, kama alivyofanya dhidi ya Ufaransa. Anataka kuona kila nchi mwanachama wa umoja wa ulaya, ikitekeleza mapatano ya mktaba wa sarafu. Kwa msimamo huu, amejitangaza huru kukabiliana na upinzani. Kwani ni katika majira ya machipuko mwakani, ambapo serikali ya Ujerumani itaidhinisha mapendekezo yote yanayohusiana na matumizi ya pesa. Hatimaye Kamishina Solbes anaidhinisha kwamba, unabidi utiliwe maanani mfumo wa mageuzi wa serikali ya Ujerumani Agenda 2010. Wakati anaposhikilia kwamba, katika mwaka huu Ujerumani haichangii uimara, basi Bw.Solbes anawafanya wanauchumi wengi kushangaa.
Gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Munich, SÜDDEUTSCHE ZETITUNG, linapotupia jicho matokeo ya mkutano mkuu wa chama-tawala cha SPD mjini Bochum, linaandika: Kansela Gerhard Schröder amefanikiwa kusahihisha mjini Bochum kile alichokuwa akidhamiria. Matokeo ya kura za kumchagua kuendelea na wadhifa wake kama mwenyekiti, yanaridhisha katika wakati mgumu kwamba, haoni haja ya kubadili mkondo wala siasa zake za binafsi na za chama. Cha pekee kinachomhangaisha, ni jinsi katibu mkuu wake Olaf Scholz alivyopata kura chache sana, ijapokuwa alithibishwa wadhifa wake. Pia anahangaishwa na matokeo yasiyoridhisha halikadhalika ya waziri wake wa uchumi Wolfgang Clement, ambaye ijapokuwa hayo amefanikiwa kusalia katika wadhifa wake. Gazeti la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER RUNDSCHAU, linaposhikilia kwamba, Kansela ndiye aliyepatwa na kishindo, linaandika: Kansela anabidi kuyatazama matokeo ya jumla ya mkutano mkuu, kama ni pigo na onyo kwa chama chake. Matarajio ya kwamba, kuanzia sasa chama chake SPD, kingenyanyuka tena katika siasa zake, yamedhihiri hayaambatani na ukweli wa hali ilivyo. Kinyume chake, kuna baadhi ya mambo, ambayo yanabidi kufanyiwa marekebisho, kuambatana na muongozo wa chama. Wajumbe hawajali kama siasa zao zinazingatia mageuzi ya kodi za matajiri na za urithi. Kile hasa wanachotaka kuona, ni ufuataji haki sawa, lakini sio mambo yanayokwenda kinyume cha hali ilivyo zama hizi. Kuhusu ziara ya siku tatu ya rais wa Marekani George W.Bush nchini Uingereza, gazeti la SCHWÄBISCHE ZEITUNG, linaandika: Vita vya Irak, vimewafanya mabwana Bush na Blair kujifunganisha pamoja kwa mnyororo, kama wangekuwa ni watumwa. Hata ikiwa Bw.Blair alitaka, hawezi kuuvunja mnyororo unaomfunganisha na ndugu yake katika silaha. Anaweza kutumaini tu kwamba, huenda ikatokea ajabu, Tony Blair anajikuta katika hali ambayo hawezi kujikomboa nayo tena, kwani hatamu nchini Irak, ziko mikononi mwa mshirika wake Bush. Iwapo wamerikani na waingereza wangefunga virago na kuondoka mara moja, basi ingetawala hali ya machafuko nchini Irak. Lakini kama washirika hawa wangesalia, basi wangewaimarisha wale wanaowapinga, hii ikimaanisha idadi ya wanajeshi wao wanaofariki kila kukicha, itazidi kupanda.