Mada muhimu zilizohaririwa na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo
8 Desemba 2003Matangazo
Kuhusu majadiliano juu ya katiba mpya ya Umoja wa Ulaya, gazeti la MANNHEIMER MORGEN, linaandika: Kila nchi mwanachama inabidi iwe ikiwakilishwa na kamishina wake binafsi. Huenda ikawa nchi za eneo la Balkan zitakuwa na mwakilishi mmoja wa pamoja mjini Brussels, lakini mbali na kwamba, mikataba ya umoja wa ulaya, haizingatii uwakilishi wa kila nchi mwanachama, hili litakuwa tatizo jipya la kuwaajiri watumnishi wapya, kuzidi kwa urasimu na hasira ya uendeshaji shuguli.
Gazeti la NEUE RUHR ZEITUNG; linapozingatia mada hii linaandika: Serikali za Warsaw na Madrid zinahisi kutopatiwa usemi mzito kutosha katika taasisi muhimu za umoja wa ulaya, tatizo ambalo huenda likatokea. Ujerumani, kwa mfano, ina raia wengi zaidi kupita Poland na Hispania kwa pamoja, lakini imepangwa kuipatia wawakilishi wawili tu. Urari wa uzito unakosekana. Ama serikali fulani inaamini katika mafungamano kati ya nchi za ulaya, au inajitoa, ulaya moja ambayo inafanana na mpangilio wa chakula, ambamo kila mojawapo kati ya nchi zote 25, inaweza kuchagua namna ya kujitangaza.
Gazeti la WIESBADENER KURIER, linaona shakashaka kuhusu swala hili linapoandika: Kile kinachodhamiriwa hapa, ni swala la kimsingi la kila nchi kuwakilishwa kidemokrasi. Haikubaliki kwa mfano kwamba, nchi kama Luxemburg yenye raia si zaidi ya 300 000, iwe na uzito sawa na nchi kama Ujerumani yenye raia zaidi ya milioni 80. Ndio maana linazuka swali, ni hadi lini Poland na Hispania zitasubiri hadi kukubaliana na ukweli huu? Kwa kila kesi katiba hii mpya ya umoja wa ulaya, haitaweza kukamilishwa hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Kwa sababu ya mashtaka yanayomkabili mwenyekiti wa shirika la ajira la Ujerumani, Florian Gerster, gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER RUNDSCHAU, linaandika: Endapo idara ya uchunguzi ya shirikisho, itathibitisha rasmi kwamba, palikuweko na makosa wakati wa kutolewa mikataba yenye thamani ya Euro Milioni 1.3, ambayo mwenyekiti wa shirika hili angewajibika kuidhinisha, basi Bw:Gerster atakutikana kuwa na hatia. Yule anayefanya kazi zisizo rasmi kwa kutumia jina la Kansela, anabidi kulaumiwa wazi hadharani. Mtumishi huyu muhimu wa Kansela Schröder, anabidi kuvua madaraka na hata yeye binafsi kuanza kutafuta ajira. Lakini kesi hii ya Bw.Gerster haihusikani na uadilifu, bali na mamlaka.
Linapozingatia mada hii kuhusiana na shirika la ajira kuwaagizia watumishi wake magari ya anasa chapa ya BMW, gazeti lingine mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLEGEMEINE, linaandika: Ni barabara kwamba, shirika hili la ajira linakiri mashtaka ya kuagiza magari hayo ya anasa, kwa kutoa hoja kwamba mikataba yake ilikuwa ya bei nafuu. Lakini hakuna mtu katika makao makuu ya shirika hili mjini Nürnberg, aliyedhania kwamba, wahusika wangeweza kufahamiwa vibaya na wauzaji wa magari hayo yatokayo mkoa wa Bavaria. Je, vipi inawezakana kwamba, shirika hili linalokabiliwa na mzigo mzito wa watu zaidi ya milioni nne wasio na kazi, linaweza kuagiza magari kama hayo ya anasa?
Gazeti la LAUSITZER RUNDSCHAU, linakamilisha uhariri katika magazeti ya Ujerumani hii leo, kwa kuzingatia mafanikio ya Ujerumani katika kutunzwa zawadi filamu yenye kichwa cha maneno: " Good bye Lenin, yaani, kwaheri Lenin" iliyotengenezwa katika Ujerumani ya Mashariki ya zamani, kwa kuandika: Mwishoni mwa wiki filamu hii na nyingine mbali mbali zilizotengenezwa katika Ujerumani, zilifanikiwa kutunzwa zawadi ya Oskar. Hili ni tukio la kihistoria lisilowahi kuonekana wakati wa kutunzwa zawadi hii barani ulaya. Hii inaweza kutazamwa kama ni rekodi mpya. Kwani ni lini filamu hii, Kwaheri Lenin, iliwahi kuvutia masilahi katika nchi zaidi ya 68? Katika Ujerumani filamu hii ilikwishatazamwa na watu zaidi ya Milioni 6 na nusu na hata inavutia masilahi ya wengi miongoni mwa watu katika nchi nyingine nyingi za ulaya.

Matangazo