Macron: Ufaransa na Poland kusaini "mkataba wa kirafiki"
29 Aprili 2025Matangazo
Poland ni mshirika mkubwa wa jirani yake Ukraine na imeonya katika miezi ya hivi karibuni kwamba huenda Moscow ikaingilia na kuvuruga uchaguzi wake wa urais wa Mei 18 mwaka huu kupitia kampeni zake za mashambulizi ya mtandaoni na taarifa potovu.
Jumatatu, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza usitishwaji wa mapigano wa upande mmoja nchini Ukraine utakaoanza Mei 8 hadi 10, hatua ambayo itakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi dhidi ya Wanazi wa Ujerumani. Hata hivyo uamuzi huo wa Putin umeibua hasira za viongozi wa Kiev ambao wameitaka Moscow kusitisha kabisa mapigano.