MigogoroUlaya
Putin na Macron wazijadili Ukraine na Iran
2 Julai 2025Matangazo
Macron ametumia mazungumzo hayo kumtolea wito Putin kusitisha vita nchini Ukraine, ingawa Putin mwenyewe alijibu kwa kuyashutumu mataifa ya magharibi kuuchochea mzozo huo.
Viongozi hao walizungumza kwa zaidi ya masaa mawili na kukubaliana kuwasiliana zaidi kuhusiana na suala la Ukraine na Iran, hii ikiwa ni kulingana na Ikulu ya Elysee.
Taarifa ya Ikulu ya Kremlin ilisema Putin alimkumbusha Macron kwamba mzozo wa Ukraine ni matokeo ya moja kwa moja ya sera za mataifa ya magharibi na kuongeza kuwa makubaliano yoyote ya amani yatatakiwa kuwa ya kina na ya muda mrefu na yatakayozingatia kuondoa kiini cha mzozo.