Macron na viongozi wa Ulaya kujadili hatma ya Ukraine
27 Machi 2025Mkutano huo unafanyika kabla ya kufikiwa makubaliano yoyote ya usitishaji vita na Urusi.
Jana rais huyo wa Ufaransa Emmanuel Macron, baada ya kuzungumza na Zelensky, alisema kuwa pendekezo la kuundwa kikosi cha Umoja wa Ulaya cha kuisadia Ukraine linaloenda sambamba na makubaliano ya amani ya baadaye, huenda likajibu shambulizi la Urusi ikiwa nchi hiyo itaishambulia nchi hiyo.
Rais Macron amesema vikosi hivyo vinaweza kupelekwa katika miji muhimu na kwingineko nchini Ukraine.
"Mbali na kuthibitisha kwamba inataka amani, Urusi inaendelea kila siku kushambulia vikali ngome za Ukraine ikiwa ni pamoja na shabaha za kiraia . Tunalaani mashambulizi hayo na lazima yakomeshwe kabisa.'' alikaririwa akisema Rais Macron.
Macron pamoja na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer wamekuwa wakishinikiza juhudi za kuunda muungano wa mataifa kwa njia moja ama nyingine kuwezesha kupelekwa kwa kikosi cha kijeshi nchini Ukraine kwa lengo la kutafuta amani ya kudumu.