Macron, Merz wasisitiza uhusiano wa karibu kati yao
29 Agosti 2025Matangazo
Pongezi hizo amezitoa Alhamisi wakati akimkaribisha Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz nchini humo.
Macron amesema baada ya miaka mingi ya uhusiano mbaya na Kansela wa zamani Olaf Scholz, kuanza upya kwa mafanikio kunaweza kutumika kama nguvu ya kuiimarisha Ulaya.
Amesema anaamini kuwa ushirikiano kati ya Ufaransa na Ujerumani sasa umeratibiwa kikamilifu ili kuanzisha Ulaya imara zaidi katika sekta za uchumi, biashara na sarafu.
Kwa upande wake, Merz amesisitiza umuhimu wa ''mhimili'' wa uhusiano wa nchi hizo mbili, akisema Ujerumani na Ufaransa zina jukumu kubwa ndani ya Umoja wa Ulaya, katika bara la Ulaya.
Merz aligusia pia jukumu muhimu la umoja na nguvu ya kweli miongoni mwa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.