Macron azuru kituo cha misaada kwa watu wa Gaza huko Misri
8 Aprili 2025Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amefanya ziara hii leo katika mji wa bandari wa El-Arish nchini Misri, kituo muhimu cha kupitisha misaada kuelekea Gaza, na kutoa wito kwa Israel kuondoa vikwazo vya kuingiza misaada ya kibinadamu katika ardhi ya Palestina inayokabiliwa na vita.
Macron, ambaye aliwasili Cairo tangu siku ya Jumapili, amesema atakutana na wagonjwa wa kipalestina na wataalamu wa afya katika kituo cha afya huko El-Arish kinachotoa msaada wa kibinadamu kwa wakazi wa Gaza.
Soma zaidi: UN: Kambi za wakimbizi Uganda zimejaa kupita kiasi
Israel ilisimamisha shughuli za kuingiza msaada kuingiaGaza mwanzoni mwa mwezi Machi, wakati wa msukosuko wa mazungumzo ya kuongeza muda wa usitishaji wa vita kati yake na kundi la Hamas na kuanzisha tena mashambulizi.
Rais Macron, Sisi wa Misri na Mfalme Abdullah II wa Jordan wote kwa pamoja wametoa mwito leo wa "kurejeshwa mara moja" kwa usitishaji mapigano ili kupunguza mateso ya watu milioni 2.4 wa Gaza.