Macron asema mashambulizi ya Israel Gaza yatasababisha maafa
20 Agosti 2025Matangazo
Katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, Macron amesema mpango huo wa Israel utalitumbukiza eneo hilo katika vita vya kudumu, akisisitiza wito wake wa ujumbe wa kimataifa wa kuleta utulivu.
Je Israel inaweza kubadili mkakati wake wa kivita, Gaza?
Wakati huo huo, mashirika ya misaada ya kimataifa, yamesema hayajaweza kupeleka misaada ya makazi katika ukanda wa Gaza licha ya mamlaka ya Israel kusema kuwa imeondoa vizuizi dhidi ya misaada.
Mashirika hayo yameonya kuwa kuendelea kuchelewa kupeleka misaada hiyo huenda kukasababisha vifo vyaWapalestina.