Macron asema atamuhimiza Trump kutoweka ushuru mpya
22 Februari 2025Matangazo
Wakati wa ziara kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Ufaransa, kabla ya mkutano wake wa Jumatatu na Trump ambaye ametishia kuweka ushuru kwa bidhaa kadhaa za Ulaya, Macron amesema atamueleza rais huyo kwamba kati ya washirika, hakupaswi kuwa na hali ya kutesana kwa kutozana ushuru.
Ulaya yasema itajibu ikiwa itawekewa ushuru na Trump
Macron pia amesema atazungumza na Trump kuhusu suala hilo kwasababu wanamuhitaji kutuliza hali hiyo, na akaongeza kuwa kilimo ni moja kati ya biashara kubwa za Ufaransa nje ya nchi.
Tangu aingie madarakani mwezi uliopita, Trump ametangaza ushuru mpya katika sekta mbalimbali, na kuzua ukosoaji kutoka kwa washirika wake Canada, Mexico, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine.