MigogoroCameroon
Macron akiri Ufaransa iliendesha vita dhidi ya Cameroon
13 Agosti 2025Matangazo
Ni mara ya kwanza kwa Ufaransa kukiri rasmi ukandamizaji wake wakati wa harakati za uhuru wa Cameroon ikiutaja kama vita.
Mwezi uliopita, Ufaransa ilituma barua kwa Rais wa Cameroon Paul Biya, kufuatia ripoti iliyotolewa mwezi Januari na Tume Maalumu ya Wanahistoria wa Kifaransa na Cameroon iliyoundwa na Macron alipozuru mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, mwaka 2022.
Wanahistoria hao walihitimisha kwamba Ufaransa iliendesha vita Cameroon na mamlaka za kikoloni zilifanya aina mbalimbali za ukandamizaji kwenye baadhi ya maeneo nchini humo.