Machafuko yameripüuka kati ya waandamanaji na vikosi vya polisi huko Edinburgh
7 Julai 2005Matangazo
Wakati huo huo machafuko makali yameripuka jana usiku kupinga mkutano wa kilele wa mataifa manane tajiri kwa viwanda.Waandamanaji Zaidi ya mia moja wamekamatwa.Kabla ya hapo mamia kadhaa ya waandamanaji walivunja senyenge zilizowekwa karibu na mahala mkutano wa viongozi unakofanyika.Vikosi vya usalama viliingilia kati na kuwatimua waandamanaji.Zaidi ya watu elfu sita wameandamana kupinga sera za viongozi wa mataifa 8 tajiri kwa viwanda.Mjini Edinburgh kwenyewe watu zaidi ya elfu tano walishiriki katika tamasha mojawapo ya mwisho ya Live 8 kuwatanabahisha walimwengu dhidi ya umasikini na maafa.