Mabomu matatu ya Vita Kuu Pili ya Dunia yagundulika Cologne
4 Juni 2025Matangazo
Inakadiriwa kuwa watu 20,000 watalazimika kuondoka katika maakazi yao mjini Cologne nchini Ujerumani mara baada ya kugunduliwa kwa mabomu matatu ya wakati wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia ili kupisha zoezi la kuyaengua mabomu hayo.
Zoezi hilo la watu kuondoka katika makaazi yao ni mojawapo ya zoezi kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni nchini Ujerumani, alisema msemaji wa mamlaka ya mji huo.
Maeneo muhimu katika mji wa Cologne ikiwemo barabara, vituo vya reli, kumbi, hospitali na nyumba za wazee zitafungwa ili kupisha zoezi hilo.
Ni muhimu kukumbuka kwamba Mji wa Cologne ni miongoni mwa miji ambayo ilishambuliwa vikali wakati wa vita vya pili vya duniani vilivyoanza mwaka 1939 na kumalizika mwaka 1945.