Mabingwa wa Afrika Al Ahly wakataa kucheza dhidi ya Zamalek
12 Machi 2025Matangazo
Ah Ahly ilisusia ikitaka maafisa wa kigeni wasimamie mechi hiyo. Mechi ilitarajiwa kuchezwa saa tatu na nusu jana usiku katika uwanja wa Cairo, lakini basi la timu liliugeza mkondo na kwenda katika uwanja ulioko karibu kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Bodi ya wakurugenzi wa klabu ilisema awali kuwa wasingecheza mchuano huo kama timu ya marefarii wa kigeni haitateuliwa. Ilidai kuwa vilabu vinatumbukizwa katika migogoro ya mara kwa mara na kiwango cha sasa cha uchezeshwaji mechi.
Ahly, ambao kwa sasa wako nafasi ya pili kwenye ligi, imesema imedhamiria kuahirisha mechi hiyo hadi pale shirikisho la kandanda la Misri EFA litakaporidhia ombi la marefa wa kigeni. EFA imekataa ombi hilo, ikitaja changamoto za muda.