Katika kuadhimisha miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili, Deutsche Welle iliitisha mdahalo jijini Dar es Salaam, Tanzania, juu ya dhima ya vyombo vya habari katika kujenga maarifa na mwamko miongoni mwa jamii.
Mohammed Khelef anaongoza mdahalo uliowashirikisha Valarie Msoka wa TAMWA, Jenerali Ulimwengu wa Raia Mwema, Assah Mwambene wa Idara ya Habari Maelezo, Maggid Mjengwa wa Mjengwa Blog, Mohammed Abdulrahmaan wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.