SiasaUturuki
Maandamano yenye vurugu yashuhudiwa Uturuki
21 Machi 2025Matangazo
Meya huyo anatazamiwa kuwa mpinzani mkuu wa rais Tayyip Erdogan katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2028.
Soma pia: Ocalan aitaka PKK kuweka chini silaha
Vurugu pia zilishuhudiwa kwenye maandamano hayo katika miji ya Istanbul, Ankara, Izmir na Eskisehir ambapo polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wenye hasira.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya ametangaza kuwa maafisa sita wa polisi wamejeruhiwa huko Istanbul, ambapo maandamano yalikuwa yamepigwa marufuku na gavana wa jimbo hilo.