Mamia ya waandishi wa habari nchini Kenya leo asubuhi walishiriki katika maandamano makubwa katikati ya mji mkuu wa Nairobi kupinga mswaada wa sheria ya kudhibiti vyombo vya habari nchini humo,lakini serikali sasa imebatilisha msimamo wake kuhusu mswaada huo wa sheria.