Maandamano ya kimataifa dhidi ya vita vya Iraq:
20 Machi 2004LONDON:
Leo ukitimiza mwaka mmoja tangu Iraq ivamiwe
kijeshi watu kote duniani wamefanya maandamano
makubwa ya kupinga vita. Maandamano makubwa
yalifanyika katika miji ya London, Roma, Tokyo
na Sydney. Pia hapa Ujerumani watu elfu kadha
waliitika mwito wa vyama vya kupigania amani na
kushiriki katika maandamano. Hata hivyo
waandalizi wa maandamano katika miji ya Berlin,
Hamburg, Frankfurt Main na Munich walitazamia
watashiriki watu wengi zaidi. Huko Filipino
yalitokea machafuko pale polisi walipowazuiya
watu wapatao 500 kufanya maandamano yao mbele
ya Ubalozi wa Marekani mjini Manila. Naye, Rais
George W. Bush wa Marekani ameikumbuka siku hii
alipoiita jamii ya kimataifa iungane katika
vita dhidi ya ugaidi. Rais Bush alisisitiza
kuwa ishara yoyote ya udhaifu au kusalimu amri
itachochea harakati hata zaidi za kigaidi.