Maandamano yamehanikiza Israel mwishoni mwa juma, raia wengi wanataka vita vikomeshwe na mateka kuachiliwa. Katika kuitizama kwa kina hali inayoendelea huko, mwenzangu Sylvia Mwehozi alizungumza na mchambuzi wa siasa za kimataifa Ibrahim Rahbi, kwanza alimuuliza maandamano haya makubwa yanatoa shinikizo kiasi gani kwa serikali ya Israel?